THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Ngoma Africa Band yawatia kiwewe wapenzi wa muziki jijini Frankfurt, Ujerumani

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band maarufu kama FFU-Ughaibuni inayoongozwa na mwanamuziki nguli Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja juzi kati ya jumamosi ya 13 Septemba 2016 ilifanikiwa tena kulitingisha jiji la Frankfurt nchini ujerumani katika maonyesho ya Afrika-Karibik Festival yaliyo fanyika katika viwanja vya Rebstock Park,ambapo bendi hiyo iliwatia kiwewe waudhuriaji wa onyesho hilo.
Bendi hiyo maarufu na mdundo wake "Bongo Dansi" inatajwa kuwa ndio bendi imara ya kiafrika kudumu kwa muda mrefu na kuteka soko la muziki barani ulaya.
 Ngoma Africa band wakishambulia jukwaa jijini Frankfurt
 Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja akiongoza gwaride la FFU Ughaibuni
 Mashabiki wa kila rika na rangi walipata kiwewe kila dakika ngoma zikipigwa
 Palikuwa hapatoshi
Kiongozi wa Ngoma Africa Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja akizongwa na mashabiki baada ya gwaride kali la FFU Ughaibuni jijini Frankfurt 


Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    FFU-Ughaibuni chini ya kamanda mti mkavu Ras makunja kiongozi wa viumbe wa ajabu Anunnaki aliens si mchezo

  2. Anonymous Anasema:

    Watoto wa mbwa aka ngoma afrika band wasio pingika kila kona mnatesa