Mwenyekiti na mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ngara wakipokea msaada wa mashuka 120 kutoka mfuko wa Taifa wa bima ya afya(NHIF)

Meneja wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akikabidhi msaada wa mashuka kwaajili ya hospital ya Nyamiyaga kwa Mwenyekiti wa halmashari ya Wilaya ya Ngara Erick Nkiramachumu.
Mkurugenzi wa halmashauri wa Wilaya ya Ngara Aidan Bahama akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa mashuka 120 kutoka mfuko wa bima ya afya,kulia ni Meneja wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera.

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) umetoa msaada wa mashuka 120 kwa hospitali ya wilaya Ngara ya Nyamiyaga kwaajili ya wagonjwa wanaolazwa hospital hapo hasa wodi ya watoto na akina mama.

Akikabidhi msaada huo, Meneja wa Mfuko wa NHIF Mkoa wa Kagera Elius Odhiambo amesema msaada huo umetolewa kutokana na mahitaji ya hospital hiyo na kuunga mkono jitihada za uongozi wa halmashauri ya wilaya za kuboresha huduma za matibabu.Odhiambo aliupongeza uongozi wa hospitali ya Nyamiyaga na halmashauri kwa kuwa na akiba ya kutosha ya dawa na vitendanishi.

"Napenda niwapongeze viongozi wa hospital hii na wa halmashauri ya Ngara kwa kuwa na akiba ya kutosha ya dawa na vitendanishi hii inawapa faraja wagonjwa kwani wanakuwa na uhakika wa matibabu na dawa wanapokuja kutibiwa pale wanapougua"alisema Odhiambo

Meneja huyo aulishauri uongozi kuufanya mpango huo wa kuweka akiba ya dawa na vitendanishi kuwa ni endelevu na kufika hadi ngazi ya zahanati na vituo vya afya.Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Ngara Erick Nkiramachumu aliushukuru mfuko wa bima ya afya (NHIF) kwa Msaada huo wa mashuka waliotoa kwani utaboresha huduma za matibabu kwa wagonjwa watakaolazwa katika hospitali hiyo.

Mwenyekiti huyo pia alizitaka hospitali za madhehebu ya Dini yaliyo na mikataba na halmashauri kutoa huduma kwa kuzingatia makubaliano yaliyo katika mikataba waliyosaini.Nkiramachumu aliahidi kuendelea kufuatilia taratibu za usajili wa hospitali ya Nyamiyaga katika mamlaka husika ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi kwa hospitali hiyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Karagwe Aidan Bahama aliahidi kuwa atasimamia kwa karibu upatikanaji wa huduma bora za tiba kwa wananchi wa hali ya chini.

"Nitasimamia kwa karibu sana upatikanaji wa huduma kwa wananchi wote,hivi karibuni nimefanya ziara za kushtukiza katika hospitali zetu ili kukagua utoaji wa huduma unavyofanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...