Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Agosti 5, 2016 amekutana na Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ukonga Jijini Dar es salaam na kuzungumza nao maswala mbalimbali ya kiusalama kwa Mkoa wa Dar es salaam, huku akiwapongeza Askari hao kwa uzalendo wao kwa Taifa.

"Hakuna wafanyakazi wazalendo nchini kama Askari, kwani wako tayari kufa ili taifa la Tanzania liwe salama, Pia uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua uhai wa mtu" alisema Makonda.

Makonda amewaahidi Askari hao kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba waimarishe usalama wa Jiji la Dar es salaam, ili iwe kama Dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta, kwani Jiji hili linapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa mkubwa.

Makonda amewahakikishia askari hao kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie katika hospitali yao huku akiahidi kufatilia ombi lake alilolitoa siku ya uzinduzi wa huduma ya polisi kwa wananchi pale viwanja vya Biafra mbele ya Mhe Rais Dkt. John Magufuli, ombi la Makonda lilikua ni juu ya asilimia 20% ya faini zinazotozwa na trafiki zibaki kwa askari ili kuboresha utendaji ikiwa ni pamoja na ukarabati wa Magari ya askari sambamba na mafuta ili polisi watakapohitajika wawe wanafika kwenye eneo la tukio bila kuchelewa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza katika Mkutano wake huo na Askari Polisi wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ukonga Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza jambo na baadhi ya Askari Polisi wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ukonga Jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. si mchezo RC Mchapakazi Makonda ndani ya kambi ya kina ras makunja wazee wa muziki mkubwa

    ReplyDelete
  2. Polisi msisumbuke na wapinzani. Hawana madhara yoyote na hawatishii amani au usalama.

    ReplyDelete
  3. Mkuu yupo vizuri kwani kawaida myu akikujengea ukuta jitahidi wewe upige plastet

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...