THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Serikali yaugomea ujenzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa SongweWaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali haitaendelea na ujenzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa Songwe uliopo mkoani Mbeya mpaka tume ya watalamu iliyoundwa kuchunguza ili kujiridhisha kama utaratibu ulizingatiwa kabla ya kuaza ujenzi huo.

Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua jengo hilo linalojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya Db Shapriya ya Tanzania ambapo amesema hadhi ya jengo hilo hairidhishi hivyo ipo haja ya kujiridhisha kama taratibu zote zilifuatwa kabla ya ujenzi.

Amebainisha kazi ya tume hiyo ya wataalamu ni kuhakiki namna utaratibu wa kumpata mkandarasi ulivyofanywa, gharama halisi za mradi na fedha iliyolipwa kwa mkandarasi kama inaendana na thamani ya jengo hilo.

"Serikali haiwezi kutoa fedha ya kumalizia jengo hili kabla ya kujiridhisha ili kuhakikisha fedha tutakazozitoa zitatumika kulingana na ilivyopangwa na thamani ya fedha inaendana na jengo lenyewe", amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha Waziri Prof. Mbarawa ameeleza  ili kuwa na miundombinu imara na ya kudumu ni lazima kuhakikisha miradi ya ujenzi wa miundombinu inasimamiwa vizuri na taratibu za kupata mkandarasi bora zinafuatwa.

"Kutokuwa na miundombinu isiyo imara ni sababu ya wahusika kuweka mbele maslahi binafsi na siyo ya Taifa", amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa Pia ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha makosa yaliyojitokezo kwenye ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza hayajirudii katika kiwanja hiki.

Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songwe Bw. Hamisi Amiri amemhakikishia Waziri Mbarawa kusimamia ujenzi uliobaki kwa kuzingatia taratibu na makubaliano yaliyowekwa ili jengo hilo lidumu kwa manufaa ya Taifa na Mkoa.

Uwanja wa Songwe ni kiungo muhimu kwa wananchi wa mikoa ya Katavi, Rukwa, Njombe na Ruvuma na katika mwaka huu wa fedha umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la abiria na taa uwanjani hapo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Shapriya Co Ltd anayejenga jengo la pili la abiria wakati alipokagua uwanja wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata ufafanuzi wa michoro ya ujenzi wa jengo la abiria kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa Songwe, Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akiendelea na ukaguzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI