Wanamuziki wa Bendi ya Sikinde Ngoma ya Ukae, wakiyarudi magoma katika Tamasha la wazi la Muziki lililofanyika kwenye Viwanja vya NAFASI, Mikocheni jijini Dar es salaam Agosti 27, 2016. Tamasha hilo ni muendelezo wa matamasha ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi katika eneo hilo, huku hilo likiwa na upekee, kwani lilihusisha uzinduzi wa Nyimbo mpya mbali mbali za Bendi tatu tofauti ambazo ni Sikinde wenyewe, Cocodo pamoja na The Spirits kutoka Bagamoyo Mkoani Pwani. Ilikuwa ni burudani ya aina yake yenye kuvutia wengi waliofika kwenye eneo hilo maarufu kwa kazi mbali mbali za Sanaa.

 Mdomo wa Bata ukipulizwa kwa ustadi wa hali ya juu na Mkongwe huyu wa Bendi ya Sikinde.
Wanamuziki wa Bendi ya The Spirits kutoka Bagamoyo Mkoani Pwani wakifanya yao jukwaani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...