Na Bashir Yakub.
Tumekuwa tukisikia fulani amepatikana na hatia ya kuua bila kukusudia au fulani ameua bila kukusudia, je unajua nini maana ya kuua bila kukusudia kisheria. Mara ya mwisho neno kuua bila kukusudia limesemwa sana baada ya hukumu katika kesi iliyohusu kifo cha mwanahabari Daudi Mwangosi. Yapo mengi ya kujua kuhusu kuua bila kukusudia.
Kifungu cha 195, sura ya 16, Kanuni za adhabu ndicho huzungumzia kuua bila kukusudia.
1.NINI MAANA YA KUUA BILA KUKUSUDIA.
Katika sheria kuua bila kukusudia (manslaughter) kunatofautishwa na kuua kwa kukusudia(murder). Kuua bila kukusudia ni kuua ambako muuaji anatenda kitendo kinachopelekea kifo lakini hakuwa na nia,dhamira au lengo la kusababisha mtu afe.
Wakati kuua kwa kukusudia ni pale mtu anapotenda tendo ambalo linapelekea mauaji ya mtu lakini amefanya hivyo akiwa amedhamiria kuua. Kwahiyo haraka utaona kuwa tofauti kubwa ya kuua kwa kukusudia na ile ya kuua bila kukusudia ni dhamira, nia au lengo.
Dhamira,nia au lengo likiwa ni kuua, basi huko ndiko kuua kwa kukusudia. Na dhamira,nia au lengo likiwa sio kuua lakini bahati mbaya mtu akafa basi hiyo itakuwa ndio kuua bila kukusudia. Tutajuaje huyu aliua kwa kukusudia na huyu hakukusudia, tutaona hapa chini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...