Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA anasikitika
kutangaza kifo cha mmoja wa watumishi wa Mamlaka, Bwana James Emmanuel
Kitainda (pichani) , kilichotokea siku ya Jumatano, tarehe 10 Agosti, 2016 jijini Dar es
Salaam baada ya kuugua kwa muda.
Bwana Kitainda alijiunga na PPRA kama
mtaalamu wa manunuzi mwezi Novemba, 2008, na alikuwa akifanya kazi kwenye Idara
ya Ufuatiliaji na Ukidhi.
Kabla ya kujiunga na PPRA, Marehemu aliwahi kufanya
kazi katika Wizara ya Fedha na Mipango katika iliyokuwa Halmashauri Kuu ya
Zabuni, kama afisa ugavi.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kuhifadhiwa
katika nyumba yake ya milele Jumamosi tarehe 13 Agosti, 2016 katika makaburi ya
Kinondoni, Dar es Salaam.
Mwenyezi
Mungu ailaze roho ya
Marehemu mahala pema peponi. Amina.
pumzika kwa amani babu!
ReplyDeleteHakika Kila Nafsi itaonja Mauti,Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea kwa wakati uliopangwa...! Pumzika kwa amani James Kitainda
ReplyDelete