Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (wa tano
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Jaji Edward
Rutakangwa, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama
ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), (wa tatu kulia), Mhe.
Shaban Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani (wa tano kushoto), Mhe.
George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (wa nne kushoto),
Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, (wa kwanza kulia), Mhe. Frederick Werema, Mwanasheria
Mkuu wa Serikali aliyemaliza muda wake (wa nne kulia), Mhe. Fakih
Jundu, Jaji Kiongozi Mstaafu (wa sita kushoto), Bw. Hussein
Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye pia ni Katibu wa
Tume ya Utumishi wa Mahakama (wa kwanza kulia), Bi. Enziel Mtei,
Katibu, Msaidizi, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Bw. Mapunda,
Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (wa pili kulia) na Bi.
Georgina Mulebya, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama,
picha hiyo ilipigwa mara baada ya zoezi fupi la kuwapongeza
waliokuwa Wajumbe wa Tume hiyo kwa kustaafu na kupandishwa
cheo iliyofanyika katika Ofisi ya Mhe. Jaji Mkuu, Mahakama ya Rufani
(T), Dar es Salaam. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kushoto)
akimkabidhi zawadi maalum kama pongezi aliyekuwa Mjumbe wa
Tume ya Utumishi wa Mahakama ambaye pia ni Jaji Kiongozi
Mstaafu, Mhe. Fakih Jundu mapema leo, zawadi hiyo imetolewa
kwake kwa kutambua mchango wake kama Mjumbe wa Tume hiyo
ya Mahakama.
Mhe. George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali akimkabidhi
zawadi maalum aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa
Mahakama, Mhe. Jaji Frederick Werema ambaye pia alikuwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, zawadi hiyo imetolewa kwake kwa
kutambua mchango wake katika Tume hiyo kipindi alichokuwa
Kamishna.
Mhe. Jaji Shaban Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani (T) (kulia)
akipokea zawadi ya pongezi kutoka kwa Bi. Georgina Mulebya,
Kamishna wa Tume ya Utuumishi wa Mahakama, zawadi hiyo
ilitolewa na Tume kwa Mhe. Lila kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa
Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), kabla ya uteuzi huo Mhe. Lila
alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...