Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella jana alikuwa mtu wa kwanza kujisajili kushiriki Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini humo.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa mbio hizo mkoani humo Bw Mongella aliekuwa ameambatana na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka, pamoja na viongozi wengine wa mchezo huo alitoa pia aliahidi kukimbia mbio za kilomita 21 ili kuonyesha nia ya dhati katika kuinua mchezo huo uliolipa taifa heshima miaka ya nyuma.

“Nitamke rasmi kwamba kwa sasa Rock City Marathon ni agenda ya mkoa na hivyo basi nitahakikisha kwamba mbio hizi zinapata washikiriki wa kutosha sambamba na wadhamini kutoka mkoa huu. Haiwezekani mbio za mkoa wa Mwanza zitegemee wadhamini wengi kutoka Dar es Salaam huku Mwanza kukiwa na makampuni na mashirika yenye uwezo wa kuusaidia mkoa wao,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw Mongella msukumo wake huo kwenye ushiriki wa mbio hizo unatokana na si tu nia ya kuinua mchezo huo mkoani mwake bali pia malengo ya mbio hizo ya kutangaza utalii wa ndani wa mkoa huo pamoja na kupinga vita ujangili hususani mauaji ya tembo.

Kwa upande wake Bw Mtaka mbali na kuwapongeza wadhamini wa mbio hizo yakiwemo mashirika ya Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust pia alitoa wito kwa makampuni mengine ya hifadhi na kitalii yafikirie kutumia fursa hiyo kutangaza utalii wa ndani.

“Pamoja na kuwapongeza waandaaji wa mbio hizi pia yaani kampuni ya Capital Plus International naomba nitoe wito kwao kuhakikisha wanaandaa utaratibu wa kuwaandaa washiriki wa mbio hizo miezi mitatu kabla kwa kuhakikisha wanapata mazoezi ya kutosha ili kama taifa tuwe na matokeo mazuri dhidi ya washiri kutoka mataifa ya nje,’’ alisisitiza.

Akizungumzia mbio hizo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema Mbio hizi zinafanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zikiwa na lengo la kusaidia utambuzi, uhamasishaji na uibuaji wa vipaji vya riadha nchini kuanzia umri mdogo kabisa sambamba na kutangaza utalii wa ndani kupitia michezo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella (alievaa kofia nyeusi) sambamba na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka ( wa kwanza kulia) wakisaini fomu za ushiriki wa Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza. Anaeshuhudia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi yam bio hizo Bw Zenno Ngowi (wa tatu kulia)
ais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi (kushoto) fomu za ushiriki wa Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya kusaini ili kuthibitisha ushiriki wake kwenye mbio hizo. Anaeshuhudia (katikati) ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella..
Mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo. Pamoja na mambo mengine Bw Mongella alielezea adhma yake ya kushirikia mbio za kilomita 21 kwenye Rock City Marathon.
Mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella ( mwenye kofia nyeusi) pamoja na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka (watatu kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji wa Rock City Marathon, wadhamini na maofisa wa michezo kutoka mkoa wa Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...