THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAKUU WA SHULE ZA MSINGI 68 KUVULIWA VYEO VYAO JIJINI DAR ES SALAAM.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum  Hapi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amewataka waalimu wa kuu wa shule  Shule za msingi 68 .
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum  Hapi.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
WALIMU wakuu wa shule 68 wa shule za Msingi wanatakiwa kuvuliwa  na kunyang'anywa vyeo vyao kwa kosa la udananyifu wa takwimu za wanafunzi  hewa tangu elimu itangazwe kuwa bure.

Hayo yamesemwa na  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum  Hapi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa walimu wakuu hao wametakiwa kuvuliwa vyeo vyao na kuwapa walimu wengine kwa kosa la kutoa takwimu za wanafunzi hewa 3462 wa shule za  msingi 68 za Wilaya ya Kinondoni. Pia hatua kali za Kisheria zitachukuliwa kwa dhidi ya walimu wakuu wa shule hizo.

Pia Hapi amemwomba Katibu Tawara wa Mkoa
kuwavua vyeo wakuu wa shule 22 wa shule za Sekondari 22 za Manispaa ya Kinondoni na Ubungo kwa kosa la kutoa takwimu za uongo na kuweka wanafunzi hewa.

Wakuu wa shule za Msingi hao wamekuwa na wanafunzi hewa 2534  kutoka shule 22 za Sekondari za Manispaa ya Kinondoni na Manispaa ya Ubungo.

Wakuu wa shule hizo wameisababishia Serikali kupoteza zaidi ya shilingi milioni 60 kwa kupeleka fedha za kuwahudumia wanafunzi wanaosoma katika shule hizo.

Baadhi ya shule za sekondari zilizokutwa na wanafunzi hewa ni Boko wanafunzi 74, Bunju B155, Goba Mpakani 42 na Hananansifu wanafunzi 154. Na shule za Sekondari ni Msisiri B wanafunzi hewa 395, Upendo 273 na Ubungo Msewe 267.