Walimu wakuu 109 kutoka shule za msingi Wilayani Serengeti wamewezeshwa mafunzo ya utumiaji wa mfumo wa taarifa za shule (School Information System - S.I.S) kwa kutumia vishikwambi (Tablet).

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofadhiliwa kupitia programu ya EQUIP Tanzania yalianza tarehe 25 Agosti na kukamilika 26 Agosti 2016 katika shule ya Msingi Kambarage iliyopo katika Mji wa Mugumu yamewawezesha walimu hao pia kupatiwa kishikwambi kwa kila mmoja.

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo, Mwezeshaji kitaifa wa Mfumo wa School Information System Bw. Victor Mkama alisema "Mafunzo hayo ni muhimu kwa walimu ili kuweza kutumia vishikwambi hivyo bila matatizo na kuwajengea uelewa wa umuhimu wa kutuma taarifa kwa kutumia njia ya mtandao".

Mwezeshaji aliendelea kwa kusema kuwa "wametoa vishikwambi 109 kwa walimu wakuu wote wa shule za msingi wilayani serengeti vyenye thamani ya Milioni 38.1 ili kuweza kutuma taarifa muhimu zinazohusu shule waliyopo moja kwa moja TAMISEMI".

Vishikwambi hivyo vitatumika katika ukusanyaji wa taarifa muhimu zikiwemo idadi ya walimu, wanafunzi, madarasa, madawati, matundu ya vyoo pamoja na nyumba za walimu na rasilimali zinazopatina katika maeneo ya shule na kutumwa moja kwa moja TAMISEMI hivyo kupunguza usumbufu wa upatikanaji wa taarifa uliokuwa ukiipata Serikali.
Mwezeshaji Kitaifa wa Mfuno wa SIS (School Information System), Deusdedit Martin akiwaelekeza baadhi ya Walimu shule za msingi Wilayani Serengeti namna ya kutumia Mfumo huo, kwa kutumia tablet.
Baadhi ya Walimu hao wakiendelea kujifunza Mfumo wa SIS.
Walimu wakielekezana namna ya kuutumia mfumo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...