Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambaye ni Mbunge wa Namtumbo Mhandisi Edwin Ngonyani anawatarifu wakazi wa Namtumbo na watanzania kwa ujumla kuwa habari iliyochapishwa kwenye gazeti la Mseto si ya kweli na ina lengo la kumchafua katika utendaji wake wa kazi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mhandisi Ngonyani amesikitishwa na taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye gazeti la Mseto la tarehe 4 Agosti 2016 ikiwa kwenye ukurasa wa kwanza yenye kichwa cha habari kilichoandikwa "WAZIRI AMCHAFUA JPM".

Habari hiyo ikiwa na nukuu "Waziri wa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kudaiwa kupokea fedha za kufanyia kampeni za ubunge kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa kuwahidi kuwa mitaji yao nchini itakuwa salama".

Aidha Mhandisi Ngonyani amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuandika habari zenye taarifa kamili na kweli ili kuepuka upotoshwaji. Habari hiyo ilikuwa imedai kuwa Mbunge huyo ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amepokea kiasi cha dolla elfu 65 kwa Bw. James Sinclair ili zimsaidie kupata nafasi ya ubunge.

Imeongeza kuwa alipewa kiasi cha dolla elfu 25 kutoka kwa Dr. Alphonce Koigi Machari ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trans Century ili apate nafasi hiyo hiyo ya ubunge.

Mhandisi Ngonyani amelitaka gazeti hilo kukanusha taarifa hiyo kwa haraka iwezekanavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...