Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Mh.Mwigulu Nchemba leo amewasili mkoani Katavi,na kufanya ukaguzi kwenye kambi ya wakimbizi ya Katumba ambako kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea nchi jirani ya Burundi na baadae kuamua kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009.

Katika ukaguzi huo, Mh. Nchemba amesema kuwa zoezi la uhakiki linafanyika ili kuchunguza mienendo yao na uwepo wao kwenye eneo la Kambi, amesema kuwa kumekuwepo na taarifa za baadhi ya ndugu zetu ambao wamekuwa wakijihusisha na watu waovu, kufanya vitendo vya kibaguzi na kutoka nje ya kambi zao na kwenda nchi jirani bila kibali.

Mbali ya kambi ya Katumba, Waziri Mwiguli alitembelea pia kambi ya Mishamo na kuviagiza vyombo vya usalama na kupitia Seririkali za mitaa kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, na kuongeza kuwa Tanzania haina tabia za kibaguzi "moja kati ya sifa kubwa ya nchi yetu ni kushinda vita dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote tangu tulipopata uhuru" alisema Mh.Mwigulu.

"Natoa rai kwa raia wote tuliowapa kibali cha kufanya kazi, kuishi na kuwa raia wa nchi yetu, waache kujihusisha na vitendo viovu na vya kibaguzi. Hatutawavumilia watu ambao tumewakaribisha kwa nia njema hapa nchini na baadae wahatarishe usalama na amani ya nchi yetu" alisema Mh. Mwigulu.

Waziri Mwigulu alikutana na Askari wa jeshi la polisi na idara zake zote na pia ametembelea gereza la mpanda ikiwa ni ziara ya kupata uhalisia wa changamoto zinazokabili jeshi la polisi, Magereza, Uhamiaji na zimamoto kwa kila mkoa,ambapo tayari kwa majawabu ya kudumu.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mh.Mwigulu Nchemba akiwapungia mkono wananchi waliopo kwenye kambi ya wakimbizi ya Katumba ambako kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea nchi jirani ya Burundi na baadae kuamua kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mh.Mwigulu Nchemba akiongozana na viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Katavi, wakati alipotembelea kambi ya wakimbizi ya Katumba ambako kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea nchi jirani ya Burundi na baadae kuamua kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jw hawakuwepo wamrushe kichura. Angewafukuza kazi. Thubutu.

    ReplyDelete
  2. Huyu ni askari wa Jeshi lipi anayepiga saluti akiwa mguu upande????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...