Waziri wa Nchi - Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira)
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba akielezea hali ya
upatikanaji wa umeme katika jimbo lake, mara Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhogo alipofanya ziara katika jimbo lake. Profesa Muhongo
yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua
miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) pamoja na
kuzungumza na wananchi.
Mbunge
wa Lushoto, Shaban Shekilindi akielezea utekelezaji wa miradi ya usambazji wa
umeme vijijini inayotekelezwa na REA katika jimbo lake mbele ya Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na wakazi wa jimbo hilo (hawapo
pichani)
Sehemu ya wakazi wa eneo la Mlola wilayani
Lushoto mkoani Tanga wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Afisa
Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zephania Maduhu (katikati) akielezea
mikakati ya ofisi yake katika kuimarisha
shughuli za uchimbaji madini katika mkoa huo. Kulia ni Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kushoto ni Mbunge wa Lushoto, Shaban
Shekilindi.
Kiongozi
wa Kikundi cha Wazee wa Utamaduni cha Mlola,
Khalfan Bakari (kushoto) akitoa maoni yake mbele ya
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo (kulia)
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akipanda mti wa
kumbukumbu katika eneo la Lukozi wilayani Lushoto mkoani Tanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...