THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

YANGA YAANZA LIGI KWA USHINDI MNONO, YAICHAPA AFRICAN LYON BAO 3-0 LEO

TIMU ya African Lyon leo imeweza kupoteza mchezo wao baada ya kukubali kipigo cha goli 3-0 kutoka kwa Yanga. Huku Kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans Van De Pluijm amesema kuwa wachezaji wake wametumia nafasi walizozipata ila mabadiliko ya kipindi cha pili yameweza kubadilisha mfumo wa ushambuliaji.
Pluijm amesifia wachezaji wake kwa kupambana katika dakika zote 90 na kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu.
Akitoa tathmini ya mchezo mzima, Pluijm amesema kuwa African Lyon ni moja ya timu nzuri na ina wachezaji wazuri sema kama wataendelea hivyo watakuwa na ushindani wa hali ya juu msimu huu.
Kwa upande wa Kocha mkuu wa African Lyon, Bernado Tevares amesema kuwa wachezaji wake walionesha kujiamini ila walishindwa kuzitumia nafasi walizozipata.
Katika mchezo wa mwanzo dhidi ya Azam, African Lyon  waliweza kutoka sare ya 1-1 huku wakionesha kandanda safi, na amewapongeza pia wachezaji wa Yanga kwa nafasi walizozipata na kuzitumia vizuri.
Katika mchezo mwingine Timu ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Toto Africa mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Deus Kaseke dakika ya 18, Saimon Msuva dakika ya 60 na Juma Mahadhi dakika ya 90.
 Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Simon Msuva, akiipatia timu yake bao la pili dhidi ya Timu ya African Lyon, katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga imeanza ligi hiyo kwa ushindi mnono wa Mabao 3-0.
 Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akitafuta namna ya kuwatoka Mabeki wa timy ya African Lyon, katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga imeanza ligi hiyo kwa ushindi mnono wa Mabao 3-0.
 Deus Kaseke wa Yanga, akishangilia baada ya kuipatia timu yake Bao la awali dhidi ya African Lyon, katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga imeanza ligi hiyo kwa ushindi mnono wa Mabao 3-0.
Mshambuliaji wa Timu ya African Lyon, Tito Okello akijaribu kutana kumtoka Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko, katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga imeanza ligi hiyo kwa ushindi mnono wa Mabao 3-0.