1
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokea kiasi cha shilingi milioni zaidi ya milioni 6 kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa Kariakoo Bw. Deo Senya wakati Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) walipofanya Harambee ya kuchangia waathirika  wa Tetemeko la Ardhi kule Bukoba mkoani Kagera ambapo Mkuu wa wilaya hiyo aliongoza harambee hiyo, Kuliani ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo na katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Kariakoo Bw.Philimin Lomano Chonde.

Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 13,708,000/= fedha taslimu zilikusanywa na vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 31564800/= jumla ya michango kwa ujumla ni shilingi milioni 45,672,800/= harambee hiyo leo ilikuwa inazinduliwa rasmi na michango inaendelea mpaka siku ya jumamosi ijayo ambapo ndiyo harambee hiyo itafungwa rasmi na wafanyabiashara mbalimbali wametakiwa kuendelea kuchangia kwa kupitia jumuiya yao ya wafanyabiashara mpaka siku ya jumamosi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokeamsaada wa viatu kutoka kwa wafanyabiashara wa kikundi cha Raha Square wafanyabiashara ambao wametoa mchango ubwa sana wa fedha na vitu mbalimbali katika harambee hiyo.
3
Wafanyabiashara wa Raha Square Kariakoo wakikabidhi mcahngo wao wa fedha kwa mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.huka na vitu vingine mbalimbali katika harambee hiyo. 
10
Mfanyabiashara Mohammed Abdallah Nofa akizungumza mara baada ya kukabidhi mchango wake wa shilingi 500,000/=  kwa Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema wa pili kutoka kulia . katika picha kulia ni Edward Mpogolo Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala na Kushoto ni Katibu wa JWK Bw. Abdallah Mwinyi
11
Wafanyabiashara kutoka Raha Square wakikusanya michango yao ya fedha taslimu na vifaa mbalimbali kabla ya kuvikabidhi leo.
12
Kiongozi wa Wafanyabiashara wauza Simu za mkononi Bw.Stanley Mwakipesile akizungumza machache mara baada ya kukabidhi mchango wao zaidi shilingi milioni 1,500,000 /=kwa mkuu wa wilaya ya Ilala katika Harambee hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...