THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DC NDEJEMBI AFANYA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA LA WILAYA YA KONGWA NAKUBAINI UFUJAJI WA PESA

Mkuu wa wilaya ya kongwa, Mh Deogratius Ndejembi amefanya kikao cha baraza la wafanya biashara wa wilaya ya kongwa, likiwa linajumuisha wafanya biashara wote wakiwamo wafanya biashara za mazao, mifugo, na biashara zingine. 

Kikao kilifunguliwa na Mh DC akiwa kama mwenyekiti wa Baraza hilo kwa nafasi yake, Mh DC Ndejembi alipokuwa akifungua kikao alisema nakusisitiza haya, Kuwa kwa mara ya kwanza yeye kama DC anafanya kikao hicho kama Mwenyekiti wa Baraza la wafanyabiashara hivo anaomba nakusisitiza ahitaji kuona Mtu anasimama nakuanza kulalamika hovyo, kama anamalalamiko aseme na kisha atoe utatuzi au maoni yakutatua hizo kero anazozilalamikia.

DC Ndejembi amefanya kikao hicho nakubaini kuna Posho nyingi na gharama kubwa sana ambazo zinatumika kwa Vikao vya Baraza hilo, ikiwemo gharama za Posho, Chakula, Uchapishaji wa nyaraka mbali mbali ambazo pia amezilalamikia kwakuwa kikao hicho kuna wajumbe wa kikao wamekosa Baadhi ya nyaraka za Vikao ambazo ukitizama Gharama za kikao hicho Wameorodhesha Machapisho na hayakuwapo ndani ya kikao lakini matumizi yanaonyesha pesa imetoka kwa ajili ya machapisho ya kikao.

DC Ndejembi amewaasa kuacha tabia zakuwa tegemezi kwani sasaivi wamekuwa wakizifuja pesa hizo kwakuwa ni Pesa zakupewa na LIC (Local  Investment Climete) kuna siku msaada huo utakwisha hivyo, waache Tabia zakulipana posho hovyo hovyo wakati vikao wanavyofanya ni vikao vyakujadili mambo yao ya msingi kwa biashara zao na kwafaida ya Taifa lao na vizazi vyao, waanze kuchangia wao wenyewe ili wawe na uchungu na pesa zao na watajadili mambo ya msingi zaidi kwakuwa na uchungu na uzalendo zaidi.
DC Ndejembi amewaeleza wafanya biashara hao kuacha Tabia za kuweka michanga na mawe katika baadhi ya mazao ambayo yanauzwa Kongwa na hasa katika Soko kuu lakimataifa la Kibaigwa! kwani ndani ya kikao hicho kuna mjumbe alisema nakukili kulalamikiwa kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kongwa na Mkoa wa Dodoma kuwa na Tabia yakujaa mawe na michanga katika mazao ili yaongezeke kilo nakujipatia faida zaidi, kitu ambacho kinasababisha soko la mazao ya ukanda huo kushuka thamani kwa michezo hiyo michafu.
Mkuu wa wilaya kaagiza kuanzia leo Atakaebainika kachanganya Mawe au Michanga katika Mazao basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.