THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DK. KIMEI ATEMBELEA MATAWI YA BENKI YA CRDB JIJINI DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei  amefanya ziara katika baadhi ya matawi ya Benki hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam kujionea utendaji kazi na kukabiliana na changamoto zilizopo. 
Katika ziara hiyo pamoja na kukagua utendaji kazi, Dk. Kimei pia alitumia fursa hiyo kukutana na kuzungumza na wateja.
Dk. Kimei pia alitembelea ATM za Benki hiyo zilipozo maeneo ya Namanga-Msasani, Mikocheni, Tegeta, Mbezi na Millennium Tower na kuahidi kuwa Benki hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa huduma hiyo inaendelea kuboreshwa ili kufikia mahitaji ya wateja. "Hivi sasa tuna zaidi ya ATMs 400 na tunajipanga kufikisha ATM 500 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.Pia aliongeza kuwa "Tumeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ATM zetu zinajazwa pesa kwa wakati ili kuondoa usumbufu wowote kwa wateja wetu" alisema Dk. Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa ziara yake katika baadhi ya matawi ili kujionea utendaji kazi pamoaja na kutembelea ATM za benki hiyo.
Dk. Charles Kimei akitoa fedha katika mashine ya ATM ya eneo la Namanga jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya ziara ya kuangalia utendaji kazi wa baadhi ya matawi ya jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, tawi la Tegeta, Richard Mkakala (kushoto), wakati alipofanya ziara kuangalia utendaji kazi katika baadhi ya matawi ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akizungumza na wateja wa benki hiyo katika tawi la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati alipofanya ziara ya kuangalia utendaji kazi katika tawi la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa tawi hilo, Wemaeli Msechu na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Tully Mwambapa.