THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KILIMANJARO QUEENS 3 vs 0 BURUNDI, ASHA RASHID NA MWANAHAMIS OMARY WAWANYANYUA MASHABIKI KAITABA

Kikosi cha Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya wanawake wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens kilichoanza leo kwenye mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki ulichezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini leo na kuibuka na ushindi wa bao 3-0.

Na Faustine Ruta, Bukoba
Bao zote za Kilimanjaro Queens zilifungwa kipindi cha kwanza, Bao la kwanza limefungwa na Asha Rashid dakika ya 22, Bao la pili lilifungwa na Mwanahamisi Omary dakika ya 30 huku

Bao la tatu lilikuwa la kujifunga wao wenyewe baada ya Mabeki wa Burundi kujichanganya na Mchezaji Niyonkulu Saidauze kwenye harakati za kutaka kuokoa mpira kwenye eneo hatari dakika ya 33. Hadi dakika 90 zinamalizika Kilimanjaro Queens ndio walikuwa wababe kwa kutoka na ushindi wa bao 3-0. Mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliokuwa ni moja ya Timu zote mbili kujiandaa na Michezo ya CECAFA Nchini Uganda. Na Kesho Timu zote mbilizinaelekea jijini Jinja, Nchini Uganda.
Kikosi cha Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya wanawake Burundi kilichoanza leo dhidi ya Kilimanjaro Queens.Timu ya Wanawake wa Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens wakiomba kabla ya Mechi kuanza.
Burundi wakipanga mbinu na kuwabana Kilimanjaro Queens punde kabla ya kipute kuanza
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu akisalimiana na Waamuzi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA