THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAKUNDI MATANO YAINGIA FAINALI YA DANCE 100% 2016 CHINI YA VODACOM TANZANIA

 Kundi la DDI Crew lililoingia fainali ya mashindano yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania ya Dance 100%,  wakishindana kwenye nusu fainali ya  mashindano  hayo katika viwanja vya Don Bosco  jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
 Wasanii wa Clever Boys ambao wameingia fainali ya mashindano yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania ya Dance 100%, wakichuana kwenye nusu fainali ya  mashindano   hayo katika viwanja vya Don Bosco  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
 Wakionyesha vipaji vyao ni kundi la Wazawa ambao wamefanikiwa kuingia fainali ya mashindano yaliyodhaminiwa na  Vodacom Tanzani ya Dance 100%, wakati wakipambana kwenye nusu fainali ya  mashindano  ya Dance 100%  katika viwanja vya Don Bosco  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kundi la Wazawa ambao wamefanikiwa kuingia fainali ya mashindano yaliyodhaminiwa na  Vodacom Tanzani ya Dance 100%
Mmoja wa Majaji wa mashindano yanayodhaminiwa na Vodacom Tanzania ya Dance100%, Super Nyamwela (kulia) akionyesha umahiri wake wa kucheza kwenye nusu fainali ya  mashindano hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Wanaoshangilia ni majaji wenzake, Lotus Kyamba  na Khalila Kellz.