THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MANJI AIPA ZAWADI YANGA SASA KUJENGA UWANJA WA KISASA.

Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa timu ya Yanga pamoja na kituo maalumu cha Kukuza vipaji vya michezo.
 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Mama Fatuma Karume wakati wa uzinduzi wa eneo la Uwanja lenye zaidi ya ekari 700 Geza Ulole lililopewa jina la Kijiji cha Yanga leo Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Mama Fatma Karume akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Kamati ya utendaji ya Yanga na wawakilishi kutoka kwa wadhamini wa timu hiyo Quality Group

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Mehboob Manji ameipatia klabu yake eneo la zaidi ya ekari 700  lilipo Geza Ulole, Kigamboni, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Kisasa.

Akiwa amewakilishwa na wasaidizi wake  wamekabidhi eneo hilo leo mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Maofisa wa chama na Serikali ya Kigamboni.

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume akiwa ameambatana na  Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Idris Katundu pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay, Sizya Lyimo na Kaimu katibu mkuu Baraka Deusdedit.

Eneo hilo lililopewa jina la Kijiji cha Yanga, rasmi utafanyika ujenzi wa kijiji cha michezo cha yanga ambapo patakuwa na uwanja wa kisasa wa mazoezi, uwanja wa mechi, hosteli na kituo cha kukuza vipaji kwa vijana pamoja na Hospital na shule.