Benchi la Ufundi la klabu ya Simba limesema hakuna kitakachowazuia kuibuka na ushindi dhidi ya Azam FC katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru.

Timu hizo mbili zitakuwa zinakutana kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu na mpaka sasa hakuna timu iliyopoteza mchezo. Simba na Azam FC mpaka sasa zimekusanya jumla ya pointi 10 kutokana na mechi nne na zimefungana kwa kila kitu kwenye msimamo huo.

Mbali ya kuwa sawa katika idadi ya mechi za kucheza, kila timu imeshinda mechi tatu, kutoka sare mechi moja, kufunga mabao saba, kufungwa mabao mawili na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Kutokana na hali hiyo, mchezo huo ndiyo utaamua nani atakuwa katika mstari mnyoofu wa kuongoza ligi na timu ipi itapoteza mwelekeo. Hii inatokana na ukweli kuwa mechi ya Simba dhidi ya Azam, Yanga dhid ya Simba na Yanga dhidi ya Azam ndizo zinazotoa hali halisi ya nani anaweza kutwaa ubingwa msimu huu.

Mayanja alisema kuwa wanajua mchezo huo utakuwa mgumu na wamejiandaa vilivyo ili kufanya vyema. Alisema kuwa Azam FC ni timu ngumu, lakini wamejidhatiti ili kuitwaa kushinda na kufuta aibu ya miaka mine ya kutotwaa ubingwa wa Tanzania Bara wala kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa kwa kushika nafasi ya pili.

“Tunajua tutakacho kifanya katika mchezo huo, tumejiandaa na jambo zuri kwetu ni kuwa tuna kikosi kipana na hakuna majeruhi hata mmoja, nawaomba mashabiki wa Simba waje kwa wingi kuipa sapoti timu yao,” alisema Mayanja.

Aliongeza kuwa wamedhamiria kukata kiu ya mashabiki wao katika mechi hiyo ambayo anaamini itakuwa njia pekee ya timu yake kufanya vyema msimu huu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...