THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said Azindua Baraza la Vijana wa Shehia Tatu za Unguja Ukuu.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said akisalimiana na Sheikh Mohammed Suleiman baada ya kusoma quran wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana Unguja Ukuu Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akionesha dhana ya ushupavu na moyo wa ujasiri wa kucheza na chatu wakati wa Uzinduzi wa Mabaraza la Vijana wa Jimbo la Tunguu Shehia za Unguja Ukuu Kaepwani, Unguja Ukuu Kaebona na Unguja Ukuu Tindini uliofanyika katika viwanja vya Idumu Unguka Ukuu leo jioni.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said akimsalimia Msanii Mussa Nyoka baada ya kutowa burudani wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Baraza la Vijana la Jimbo hilo. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akiwa na simu wakati Mhe Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Anayeshughulikia Muungano Mhe. January Makamba akiongea na Wananchi akiwa Mjini Dodoma alikuwa ahudhuria uzinduzi huo wa Mabaraza la Vijana wa Shehia za Unguja Ukuu Zanzibar na kutoa ahadi ya kuchangia shilingi milioni tatu kwa Shehia hizo Tatu za Unguja Ukuu Kaepwani. Unguja Ukuu Kaebona na Unguja Ukuu Tindini.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akizungumza nma Viongozi wa Mabaraza ya Vijana ya Shehia za Unguja Ukuu wakati wa kumalizika kwa hafla hiyo ya Uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya mpira vya Idumu Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja.