Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii.

TIMU ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imeanza mazoezi kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Congo Brazaville unaotarajiwa kupigwa Jumapili ya Septemba 18 kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo wa mwisho kwa Serengeti Boys utakuwa wa umuhimu mkubwa sana kwani watahitaji ushindi wa hali yoyote ile ili kuweza kufuzu kuingia kwenye kombe la Mataifa Afrika kwa Vijana 2017 yatakayofanyika Nchini  Madagascar.
Kikosi  hicho kiliweka kambi ya takribani wiki moja katika visiwa vya Shelisheli iliweza kucheza mchezo mmoja wa Kirafiki na timu ya Dynamo na kufanikiwa kutoka na ushindi.
Akizungumza na Michuzi Blog, Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF, Alfred Lucas amesema kuwa kikosi cha Serengeti Boys kimejizatiti kuweza kuhakikisha wanapata ushindi ili kuweka mazingira ya kwenda fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana.
Lucas amesema, wana imani na kikosi hicgo na zaidi wameshacheza michezo kadhaa na hawajapoteza hata mechi moja kwahiyo Kocha Mkuu wa yimu hiyo Bakari Shime ameendelea kuwapa mbinu mbalimbali ili kuweza kutoka na ushindi kwenye mchezo huo.
Kwa upande wa msafara wa timu ya Congo Brazavlle , Lucas amesema utakuja na watu 40 ambapo unatarajiwa kuingia kesho saa 7:45 mchana huku waamuzi wakitarajiwa kuingia Ijumaa, na kikosi cha Congo Brazaville kitafanya mazoezi kesho ijumaa kwenye Uwanja wa Karume na siku ya Jumamosi Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo utachezwa majira ya saa 10 jioni na watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kuja kuisapoti timu yao ili iweze kufanya vizuri na kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Vijana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...