THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Serikali kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium LukuviNa 
 
 
 

Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma

Serikali imesema imejipanga kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi inayotokana na wathamini kutozingatia maadili ya uthamini pamoja na kazi za uthamini kufanywa na watu wasiokuwa na sifa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi leo mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini mwaka 2016 katika mkutano wa nne wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Lukuvi amesema kuwa lengo kuu la Muswada huo ni kutunga Sheria itakayoweza kusimamia taaluma na shughuli za uthamini Tanzania Bara kwa kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii na sekta ya ardhi kwa ujumla.

Aidha, Waziri huyo amesema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa itasaidia katika kuwaondolea mateso wananchi wanaothaminiwa mali zao na kuchelewa kulipwa fidia kwa kuweka ukomo wa muda ambao fidia hiyo lazima ilipwe na kuwadhibiti wawekezaji kulipa fidia kwa wakati.

Pia ameongeza kuwa sharia hiyo itasaidia kuondoa utapeli uliokuwa unafanywa na wathamini kuongeza thamani kinyume na utaratibu na kuongeza wafidiwa hewa sambamba na kuthibiti uthamini wa kifisadi ambao umekuwa ukifanywa na wathamini kwa kushusha thamani ya mali kwa madhumuni ya kukwepa kulipa kodi.

Zaidi ya hayo, katika usajili wa wathamini chini ya sheria hiyo inayopendekezwa, kutakuwa na mfumo wa kuwawajibisha wathamini ambao watakaokiuka maadili ya kitaaluma, kutoa adhabu kwa wathamini wanaokiuka sharia hiyo ikiwa ni pamoja na kifungo, faini kali na kusimamishwa au kufutiwa usajili.

Kwa upande wake Waziri Kivuli kambi ya upinzani katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wilfred Lwakatare amesema kuwa sheria hiyo ikitekelezwa itasaidia kupunguza changamoto katika sekta ya ardhi na nyumba zilizokuwa zinatokana na matatizo ya uthamini.