Na:
Genofeva Matemu – WHUSM
Serikali
ipo tayari kuendeleza michezo yote badala ya kubaki na michezo michache ikiwemo
mchezo wa mpira wa magongo (Hockey) ambao kwa miaka mingi iliyopita mchezo huo
uliiletea heshima kubwa Tanzania.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye wakati wa ziara ya marais wa shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo
Duniani na Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
“Mchezo
wa mpira wa magongo ni mchezo ambao Tanzania kwa miaka mingi iliyopita
ulituletea heshima kubwa hivyo kwa ujio ziara ya marais wa shirikisho la Mpira
wa Magongo (Hockey) Duniani na Afrika itasaidia kuurejesha mchezo huo kwenye hadhi
yake”, alisema Mhe. Nnauye.
Mhe.
Nape Nnauye amesema kuwa Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) ni moja ya michezo
ambayo inachezwa sana kwenye mishindano ya Olympic hivyo kama Tanzania itafanya
maandalizi ya kutosha pengine Olympic ijayo ikapata fursa ya kuwa na wachezaji
wa Hockey ambao watashiriki Olympic na kuiwezesha kupata medali za mchezo huo.
Naye
Rais wa mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Duniani Bw. Leandro Negre ameahidi
kusaidia miundombinu ya mchezo huo hasa uwanja kurejesha jitihada zinazofanywa
na Tanzania huku akiiomba serikali kuipatia ardhi itakayowawezesha kujenga
uwanja mzuri na wa kisasa kupitia shirikisho la mchezo wa mpira wa magongo
duniani.
Aidha
Rais wa Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Afrika Bw. Seif Ahmed ameahidi kuongeza
miundombinu katika uwanja wa kisasa utakaojengwa na shirikisho la mchezo wa
mpira wa magongo duniani nchini Tanzania kwa kuuwekea miundombinu muhimu
ikiwemo mataa na vitu vingine ili kuhakikisha uwanja huo unakua na hadhi ya
kuchezwa michezo ya kimataifa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa naMichezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akiangalia zawadi aliyopokea kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Duniani Bw. Leandro Negre(Kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu maendeleo ya mchezo wa Hockey Tanzania kulia ni Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Afrika Bw. Seif Ahmed Septemba 21,2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi (hawapo Pichani) kuhusu ujio wa Rais wa Rais wa Shirikisho Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Duniani kushirikiana na Tanzania kuendeleza mchezo wa Hockey Tanzania kulia ni Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Duniani Bw. Leandro Negre na kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Afrika Bw. Seif Ahmed Septemba 21,2016.
Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Duniani Bw. Leandro Negre akizungumza na waandishi (hawapo Pichani) kuhusu ujio wake na mpingo yake ya kushirikiana na Tanzania kuendeleza Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Tanzania kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa naMichezo Mhe. Nape Moses Nnauye Septemba 21,2016.
Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Afrika Bw. Seif Ahmed akizungumza na waandishi (hawapo Pichani) kuhusu ujio wa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Duniani mipango yao kushirikiana na Tanzania kuendeleza Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Tanzania kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa naMichezo Mhe. Nape Moses Nnauye Septemba 21,2016.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...