Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Iddi Mgaza wa Pili kutoka kulia akipata chakula cha pamoja na viongozi wa vikundi mbalimbali vya mahujaji kutoka Tanzania katika mojawapo ya makazi ya mahujaji mjini Makkah. Wa tatu kutoka kulia ni Rais wa vikundi vyote vya Mahujaji BIITHA Sheikh Abdallah Talib, wa kwanza kushoto ni Rais wa taasisi za Hijja kutoka Zanzibar UTAHIZA Sheikh Ali Adam na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Utawala Ubalozini Bw. Ahmada Sufiani Ali.
Viongozi na mahujaji wakiendelea kupata chakula cha pamoja.

Mahujaji wa kutoka Tanzania wapatao 2,000 waliwasili salama katika miji mitakatifu ya Makkah na Madina mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu na tayari wameshaanza kufanya ibada pamoja na ziara hadi katikati ya mwezi Septemba mwaka huu.

Hakuna taarifa zozote za matatizo kuhusu mahujaji wa Tanzania katika maeneo waliyofikia, wote wako salama na afya njema.

Mwaka huu Serikali ya Saudi Arabia imeimarisha miundo mbinu, usafiri, ulinzi, usalama na uangalizi makini kuhakikisha kuwa hakuna dosari zozote zinazoweza kutokea kutokana na uwepo wa wingi wa mahujaji kutoka nchi mbalimbali duniani. Takriban mahujaji milioni 2 kutoka mabara yote duniani wapo nchini Saudi Arabia kutekeleza nguzo mojawapo kati ya nguzo 5 za dini ya kiislamu.

Taarifa imetolewa na:
Balozi Hemedi Iddi Mgaza
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...