THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TAARIFA KWA WANA-DIASPORA/WATANZANIA KUHUSU JUHUDI ZA KUCHANGIA MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA- TANZANIA


Ndugu Watanzania wanaoishi nchini Uingereza na wana-Diaspora wote popote pale mlipo. Salaam.
Kamati ya Mpito ya Jumuiya ya Watanzania/Wana-Diaspora Uingereza,inaitikia wito wa serikali na inapenda kuwajulisha kuwa inaendelea na juhudi za kuwashirikisha Watanzania na marafiki wa Watanzania duniani kote katika kuchangia maafa yaliyowapata ndugu zetu wa mkoa wa Kagera na maeneo jirani yaliyokumbwa na maafa . 
Taarifa kutoka vyombo vya habari zinaonesha kuwa mpaka sasa ndugu zetu 20 wamepoteza maisha, na wengine wengi  wanahitaji huduma mbali mbali za kiafya na kijamii, hususa ni matibabu na makazi ya kudumu. 
Tumependekeza utaratibu wa kuchangia kwa njia ya mtandao ili kurahisisha uchangiaji na kuweka uwazi katika kufuatilia maendeleo ya michango. Tunawaomba Watanzania wote na marafiki wa Watanzania walioguswa na maafa haya, tuchangie kwa hali na mali kupitia kwenye tovuti hii hapa chini na michango hii itawakilishwa moja kwa moja kwa kamati ya maafa ofisi ya waziri mkuu mara zoezi litakapokamilika.
 Njia hii itarahisisha kupunguza gharama za “international transaction money transfer fee” hasa kwa wanadiaspora na marafiki zao wanaotaka kuchangia kwa kiasi kidogo kidogo kama £10, $10, or 10 euro nk. Idadi ya watu wa namna hii ni kubwa sana, ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha zoezi hili. 
Kamati ya mpito inawajulisha Watanzania wote waishio Uingereza kuwa hivi karibuni ilialikwa Ubalozini na kukutana na Balozi wetu Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro. Maongezi yalikuwa mazuri na bado yanaendelea. 
Kwa sasa tunawaomba tuungane kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu, wale wote waliopoteza maisha yao na pia, kuwaombea majeruhi ili wapone haraka. Tunawaomba sana tujitoe kwa hali na mali kuwachangia ndugu zetu katika kipindi hiki kigumu.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu atuzidishie moyo 
wa upendo ili “Tuwapende Majirani zetu kama Tunavyojipenda”.

Ili kuchangia bonyeza link hapa chini


Mungu Ibariki Tanzania.

Eng. Dr Julius Hingira                                                                        Abraham Sangiwa                                                                
Mwenyekiti – Kamati ya Mpito.                                                         Katibu Mkuu – Kamati ya Mpito

TZUK DIASPORA / TANZUK                                                              TZUK DIASPORA / TANZUK