Kampuni ya Ubongo imezindua albam mbili za nyimbo za  kufundishia watoto kutoka kwenye vipindi vyake pendwa vya “Akili and Me” na “Ubongo Kids”. Albamu hizi zimezinduliwa ili kuendelea kuhakikisha kuwa watoto wa Tanzania na Afrika kwa ujumla wanaendelea  kufurahia na kujifunza kupitia kazi zenye maudhui ya Kiafrika.

Albamu ya “Hisabati ni mikakati” ni mahususi kwaajili ya watoto wa umri wa miaka 7-14 lakini familia nzima inaweza kusikiliza na kufurahia. Albamu hii itampa nafasi msikilizaji kusikiliza nyimbo nzuri toka kwa wahusika wa Ubongo Kids akiwemo Mama Ndege, Anko T na  Toto Tembo. Nyimbo zilizopo ni pamoja na “Hisabati Ni Mikakati”, “Sifuri ni Nini” na wimbo wenye mahadhi ya taarab uitwao “Desimali Ni Rahisi”. 

Kwa wasikilizaji wenye umri chini ya miaka 7 watapata nafasi ya kuimba, kuruka na kufurahia pamoja na Akili na rafiki zake. Watajifunza kuhesabu kwenye wimbo wa “Vidole Vitano”,  maumbo kama “Mraba” na “Pembetatu” pamoja na kujifunza sehemu za mwili kwenye wimbo wa “Nikisema”.  

Mtayarishaji wa albam hizi, Bi. Alicia Simba, amesema “Watoto wa Kitanzania hawana nyimbo zilizotengenezwa mahususi kwaajili yao, na kampuni ya Ubongo inajitahidi kuondoa hali hii. Lengo letu ni kuzidi kuwaelimisha na kuwaburudisha watoto wa Kiafrika huku tukihakikisha kuwa wanajivunia uafrika wao. Zaidi ya yote, nyimbo hizi zipo kwa lugha ya Kiingereza pia hivyo tunaamini zitawasaidia watoto kujifunza Kiingereza na zitafanya vizuri hata nje ya bara la Afrika.’’

Unaweza kuzipata albamu hizi kupitia Apple Music, iTunes, Spotify, Amazon Music na  Deezer. Unaweza kudownload singo za albam hizi kupitia www.ubongokids.com/music na www.akiliandme.com/music bure kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...