Mwenyekiti
wa Chama cha CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Mbowe
Na Anthony John,
Globu ya Jamii
Globu ya Jamii
Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha shughuli zote za
maandamano na mikutano nchi nzima,kwa kudai kuwa ukuta ni fikra endelevu na si mpango
wa siku moja.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti
wa Chama hicho Taifa,Mh.Freeman Mbowe wakati akizungumza
na Waandishi wa Habari,Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Mbowe amesema kuwa wataendelea Kujipanga katika kulinda Haki yao ya kidemokrasia kama ambavyo katiba
ya vyama vya siasa inavyosema,kuwa ni haki yao ya kidemokrasia.
‘’Mapambano ya kisiasa si tukio la siku moja ni tukio
endelevu na kwa hiyo tarehi Mossi ,Oktoba ambayo ilikuwa ni siku mbadala ya maandamano
maalum,hivyo kwa niaba ya kamati kuu imeona kuna umuhimu wa kusimamisha maandamano maalumu na mikutano
nchi nzima ilikupisha mbinu nyingine mbalimbali’’amesema Mbowe
Njaa zinasumbua sana vichwa vya watu. Angalau leo umempa sekunde 20.
ReplyDeleteHizo njaa zisituchafulie nchi basi. hawa jamaa wa kusini wana agenda nyingine. Mbona Moshi mjini kutulivu na hawafanyi fujo huko?
ReplyDeletehakuna maandamano. Mnatishia nyau tingatinga?? Acheni kuwaongepea wananchi hakuna cha maandamano.
ReplyDeleteMbona magazeti ya Tanzania yanapenda uchochezi baina ya serikali Na upinzani baada ya kuandika maneno ya kuwapongeza wanatia vitina sio sawa
Delete