THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UNESCO YAZINDUA RIPOTI YA UFUATILIAJI WA ELIMU DUNIANI (GEM) 2016

 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akielezea siku ya kisomo duniani na dhumuni la UNESCO kuanzisha siku hiyo.

Na Mwandishi wetu
Katika kutambua umuhimu wa kusoma na kuandika Tanzania na mataifa mengine duniani zimeungana kwa pamoja kuadhimisha siku ya Kisomo Duniani ambayo huadhimishwa kila Septemba, 8 ya kila mwaka ambapo pamoja na maadhimisho hayo pia iliambatana na Uzinduzi wa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani (GEM).

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez alisema kuwa dhumuni la UNESCO kuweka siku hii ya Septemba 8 kila mwaka kuwa siku ya kisomo kimataifa ili kuziunganisha jamii zote za kimataifa duniani kuweka na kuendeleza nguvu na juhudi kwa watu kujua kusoma na kuandika ili kuleta maendeleo katika jamii mbalimbali.

“Kauli mbiu hii inatufungulia milango ya uelewa juu ya malengo na mafanikio ya miongo mitano iliyopita ambayo yaliwekwa ya kutaka kila mtu anajua kusoma,” alisema Bi. Rodrieguez na kuongeza.“Tunataka kujua ni changamoto gani zinazoikabili sekta ya elimu katika kusoma na kuandika na tunataka kufahamu namna ya kukabiliana na changamoto hizo ili kufikia malengo ambayo UNESCO iliyakusudia kufikiwa ya kila mmoja awe anajua kusoma.”
 Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta akizungumzia juhudi za serikali za kuhakikisha kila mtanzania anajua kusoma.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI