Dar
es Salaam, TANZANIA – Leo katika Ofisi za Wamarekani wa Kujitolea, Kaimu Balozi
wa Marekani nchini Virginia Blaser amewaapisha wafanyakazi wa kujitolea wa
Kimarekani (Peace Corps Volunteers) wapatao 51 ili kuanza huduma yao ya miaka
miwili.
Wafanyakazi hawa wa kujitolea wa Kimarekani watafanya kazi katika sekta
ya elimu. Mwaka uliopita katika Programu ya Elimu, wafanyakazi wa kujitolea wa
Peace Corps 110 walifundisha katika shule za sekondari 108 katika mikoa 22 kwenye
zaidi ya wilaya 30 nchini Tanzania na kuwafikia takriban wanafunzi 36,000. Hawa wafanyakazi wa kujitolea 51 wanaungana
na wengine 195 ambao tayari wako nchini wakifanya kazi katika elimu ya
sekondari (hisabati, sayansi na kiingereza), kukuza sekta ya afya, na elimu ya
mazingira.
Mheshimiwa Salum S.
Salum, Afisa Elimu Mkuu, aliiwakilisha wizara ya elimu katika hafla ya uapisho.
Hafla hii ilihudhuriwa pia na wafanyakazi wengine wa kujitolea wanaoendelea
kuhudumu na wale waliomaliza muda wao pamoja na maafisa kutoka taasisi wabia.
Mbali
na kufundisha madarasani nchini kote, wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps
hushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii. Shughuli hizi ni kama
kusaidia kuboresha maktaba za shule, kuandaa programu za kukuza uelewa wa VVU/UKIMWI,
na kukuza stadi za maisha za wanafunzi. Wafanyakazi wa kujitolea walioapishwa
leo, watapangiwa kufanya kazi katika wilaya zifuatazo nchini kote: Karatu,
Kongwa, Chamwino, Mufindi, Iringa Rural, Hai, Rungwe, Lushoto, Wete, Nzega,
Sumbawanga, Same, Ruangwa, Nachingwea, Hanang, Babati, Kiteto, Busokelo, Kyela,
Chunya, Mbarali, Masasi, Newala, Mtwara rural, Mbinga, Morogoro Manispaa,
Shinyanga, Kishapu, Maswa, Wanging’ombe, Singida, Njombe, Nzega na Lushoto.
"Wiki
hii inaadhimisha miaka 55 ya kupitishwa kwa sheria ya Peace Corps, ambayo
ilianzisha rasmi taasisi ya Peace Corps mwaka 1961. Kuwaapisha hawa wafanyakazi
wa kujitolea katika maadhimisho haya maalum ni ishara ya kielelezo muhimu ya
ushirikiano kati ya watu-kwa-watu ambao Peace Corps inahamasisha nchini
Tanzania,” alisema Kaimu Balozi wa Marekani Virginia Blaser.
Zaidi ya Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps wapatao 2,000
wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1962. Peace Corps hutoa mafunzo kwa
wafanyakazi wa kujitolea wa Marekani wanao fanyakazi katika jamii katika nyanja
za elimu ya sekondari (wakifundisha hisabati, sayansi na teknolojia ya
mawasilianoa), afya na elimu ya mazingira.
Peace Corps ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na
Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi
wa kujitolea zaidi ya 7,000 katika zaidi ya nchi 70 duniani. Kwa miaka 50,
Peace Corps imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi
na kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini.
Peace Corps ina
dhamira ya kukuza amani na urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu
yafuatayo:
·
Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani watakaochangia kuleta
maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi itakayohitaji wafanyakazi hao;
·
Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu katika jamii
zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea;
·
Kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na watu wake.
Zaidi ya Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps wapatao 2,000
wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1962. Peace Corps hutoa mafunzo kwa
wafanyakazi wa kujitolea wa Marekani wanao fanyakazi katika jamii katika Nyanja
za elimu ya sekondari (wakifundisha hisabati, sayansi na teknolojia ya
mawasilianoa), afya na elimu ya mazingira.
Sehemu ya wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani (Peace Corps Volunteers) wapatao 51 wakila kiapo ili kuanza huduma yao ya miaka miwili leo katika Ofisi za Wamarekani wa Kujitolea jijini Dar es salaam. Picha kwa hisani ya Ubalozi wa Marekani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...