WAFANYAKAZI wa Mathayo Suleiman Foundation wachangia Dam katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Mathayo Suleiman Foundation ni foundation inayojihusisha na kutoa huduma kwa maendeleo ya jamii na kuwaunganisha wanawake pamoja na vijana katika shughuli za uzalishaji mali.

Pia na Foundation Inayosaidia vikundi vyenye shida na mahitaji maalumu kama watoto yatima.

Mwenyekiti Mtendaji wa Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaphy Mathayo akizungumza na wafanyakazi hao amesema kuwa leongo kuu la kuchangia damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni kuokoa maisha ya wahitaji wa damu wanaofikishwa katika hospitali hiyo.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaphy Mathayo akizungumza kabla ya kuingia kuchangia Damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa lengo la kuchangia damu katika Hospitali ya Taifa ni kuokoa maisha ya watu wenye mahitaji ya kuongezewa damu.
 Mratibu wa Mathayo Suleiman Foundation, Banga Suleiman akizungumza na wafanyakazi wa Foundation hiyo pamoja na kuwashukuru Wafanyakazi wa Mathayo Suleiman Foundation jinsi walivyojitoa katika kusaidia na kuokoa maisha ya watu wenye mahitaji ya kuongezewa damu katika hospitali ya Mhimbili jijini Dar es Salaam leo. 
 Mwenyekiti Mtendaji wa Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaphy Mathayo  akizungumza na mtoa huduma wakati akiendelea kuchangia damu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...