THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WASANII WA KITANZANIA WANAIOSHI UINGEREZA WAKUTANA NA BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO

Kundi la wasanii wanane  wa Kitanzania waishio nchini Unigereza (Wasanii Tanzania Uingereza - WASATU) waliwakilisha wenzao  Jumatano iliyopita katika kikao na Balozi mpya wa Tanzania nchini humo  Dkt. Asha-Rose Migiro.
Kikao  hicho kilichoitishwa  na mheshimiwa Balozi kilikuwa na madhumuni  ya kuweka ushirikiano kati ya jumuiya ya wasanii na Watanzania na Ubalozi huo. Balozi Migiro alisisitiza kuwa sera ya awamu ya tano ni kuipa sanaa kipaumbele ili kuchangia maendeleo yetu ndani na nje.
Wasanii hao walioongozwa na mcheza sarakasi na mwanamuziki Fab Moses walijitolea bila malipo yeyote – wengine kutoka safari za mbali sana.
WASATU  ilisisitiza haja ya kujituma zaidi kujenga sanaa na mawasiliano na kusaidiana kujuana kuendeleza fani hii muhimu.
 Kutoka kushoto , Rama Sax – aliyekuwa bendi ya Simba wa Nyika zamani, Saidi Kanda aliyepiga na marehemu Remmy Ongala, Hamida Mbaga wa All Things African, Khadija Ismail wa Kibisa na Muungano ya enzi hizo,  Balozi Dkt Asha Rose Migiro, Neema Kitilya anayetangaza mapishi ya Kitanzania Uingereza na mwanamuziki Msafiri aliyewahi kuwa na African Stars band wana Twanga Pepeta ambaye siku hizi anatumia jina la Diouf Lewandowski. Waliochuchumaa mbele ni Freddy Macha na Fab Moses
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza  Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na msanii Hamida Mbaga wa All Things African
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza  Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na msanii, mwandishi na mwanaharakati wa utamaduni Freddy Macha
   Balozi wa Tanzania nchini Uingereza  Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa  na mwanamuziki Msafiri a.k.a Diouf Lewandowski
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza  Dkt. Asha-Rose Migiro akiongea na wasanii hao