THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako ziarani Kigoma

Na Abel Daud wa Globu ya Jamii, Kigoma
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewahakikishia wanafunzi kote nchini kwamba Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha inatengeneza mazingira rafiki ili kila atakayefaulu aweze kuendelea na hatua ya juu zaidi ya kielimu. 
Hayo ameyasema leo hii Wilayani Kasulu alipotembelea Shule ya Msingi Mwenge pamoja na Chuo cha Elimu ya Taifa Kasulu kukagua miundombinu tayari kwa kupokea wanafunzi wa diploma kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma maarufu kama UDOM. 
 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi amemueleza Waziri Ndalichako kuwa Wilaya yake imejipanga kuinua elimu kwa kiwango kikubwa na kuwataka watumishi wa halmashauri za Kasulu pamoja na wananchi kwa ujumla kumpa ushirikiano ili kufikia malengo waliyojipangia ya kuinua elimu wilayani hapo. 
 Prof.Ndalichako ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Kasulu kwa kubuni mkakati endelevu wa kuinua elimu wilaya humo  na kuwataka kusimamia swala hilo kwa vitendo.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali Martin Mkisi   wakikagua miundombinu ya Chuo cha Elimu ya Taifa Kasulu tayari kwa mapokezi ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma - UDOM - wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri mkoani humo leo
 WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali Martin Mkisi   wakikagua miundombinu ya Chuo cha Elimu ya Taifa Kasulu  
 WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali Martin Mkisi  wakikagua ufanyaji wa mitihani ya Darasa la saba 2016 katika  Shule ya Msingi Mwenge, Kasulu.
 WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali Martin Mkisi   wakikagua  ufanyaji wa mitihani ya Darasa la saba 2016 katika Shule ya Msingi Mwenge, Kasulu.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiskiliza taarifa ya elimu kutoka kwa  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali Martin Mkisi wakati wa ziara ya mkoa wa huo leo.