THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

ARUSHA OPEN YAMALIZIKA LUGALO YANYAKUA NAFASI TANO KATI YA 13 SAWA NA ASILIMIA 53

Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ

Mashindano ya Wazi ya Golf Arusha open yamemalizika jijini Arusha Oktoba 16 huku Timu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo ikifanya vizuri kwa kunyakua ushindi katika makundi kwa asilimia 53 huku ushindi wa Jumla ukichukuliwa na Mchezaji kutoka klabu ya Kilimanjaro.

Mpiga golf wa Timu ya Kilimanjaro issack Wanyeche akiibuka mshindi wa jumla wa mashindano hayo yaliyokuwa yakishindanishwa kwa mtindo wa Mikwaju ya Jumla Net kwenye makundi na Gross kwa ushindi wa Jumla.

Katika Division A Mshindi ni kapteni Shaaban Kibuna kutoka Klabu ya Liugalo akifuatiwa na Richard Mtweve naye wa Lugalo ambaye walifungana kwa Mikwaju ya Jumla 145 kila mmoja lakini kutokana na kapteni kibuna kucheza vizuri siku ya mwisho akamshinda Mtweve kutokana na kucheza net ya 70 kwa 75 wakatik siku ya kwanza ilikuwa 75 kwa 70 ya Mtweve.

Kundi B ambalo Timu ya Lugalo haikuingiza mchezaji katika kundi hilol imechukuliwa na N Matsouka wa Arusha aliyepata mikwaju ya Jumla 143 akifuatiwa na mshindi wa pili ni Musadiq Versi aliyepiga mikwaju ya Jumla 147.
Divisheni C Mshindi ni Talib Chagani aliyepiga Mikwaju ya Jumla 148 akifuatiwa na kapteni Amanzi Mandengule wa lugalo aliyepiga mikwaju ya jumla 149.

Kwa upande wa Kundi la wadogo Junior mshindi ni Almadiuos Simon kutoka Klabu ya Jeshi ya Lugalo kwa kupiga Mikwaju ya Jumla 131 huku mshindi wa Siku ya kwanza ni Salim Sharif aliyepata Net ya 70 na Mshindi wa Siku ya Pili ni Clemence Mutavangu wa Lugalo aliyepiga Net ya 69.

Kwa Upande wake Nahodha wa Klabu ya jeshi ya Lugalo ambaye ni Mshindi wa Divisheni A kapten Shaban Kibuna amesema wamefanya vizuri kutokana kuingiza wachezaji 14 na kunyakua nafasi tano ukilinganisha na Arusha waliongiza wachezaji zaidi ya 50 na TPC walioingiza wachezaji 17 na kutoka bila ushindi.

Alisema kinachofuata sasa ni klabu yake kujiandaa na mashindano yaliyoko mbele yao ya Oktoba 22 Mwaka huu lakini pia wanatarajiwa kuwa na mshindano ya Waitara Trophy na Miaka 10 ya Klabu mwezi Desemba.
Mshindi wa Kwanza wea Division A wa Mashindano ya Wazi ya Arusha Open Kapten Shaban Kibuna akiwa katika harakati za mchezo huo katika mashindano yaliyomalizika Jumapili Oktoba 16 Jijini Arusha .(Picha na Luteni Selemani Semunyu). 
Mshindi wa Kwanza wa kundi la Wadogo Junior wa Mashindano ya Wazi ya Arusha Open Almadious Simon akiwa katika harakati za mchezo huo katika mashindano yaliyomalizika Jumapili Oktoba 16 Jijini Arusha .(Picha na Luteni Selemani Semunyu). 
Mchezaji wa Golf wa Timu ya JWTZ ya Lugalo Nicholous Chitanda akiwa katika harakati za Mashindano ya Wazi ya Arusha Open katika mashindano yaliyomalizika Jumapili Oktoba 16 Jijini Arusha .(Picha na Luteni Selemani Semunyu).