Na Daudi
Manongi-MAELEZO.
Kampuni ya Ndege Tanzania
(ATCL) imetoa ofa ya mwezi mmoja kwa abira wanaosafiri kutoka Dar es salaam
kwenda Mwanza kulipa nauli ya shilingi 160,000/- kwa safari moja.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es salaam na na Kaimu Afisa Mawasiliano wa Kampuni Bi.Lily
Fungamtama wakati akiongea na Idara ya Habari.
Amesema Ndege za
Kampuni zimeanza kutoa huduma kuanzia Jumamosi ya wiki iliyopita ya tarehe 15
ya mwezi huu kama ilivyobainisha kupitia vyombo vya Habari.
Safari hizo zilianza kwa
kutoa huduma ya kusafirisha abiria kuelekea nchini Comoro na hapa nchini itoa
safari katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Kigoma.
Bi.Fungamtama amesema
kwa kuanzia walianza na mazoezi ya vitendo kwa marubani na wafanyakazi wa ndani
ya Ndege ambapo hatimaye walianza safari za biashara ya kusafirisha abiria mnamo
tarehe 15 Oktoba kama ilivyopangwa.
Ameongeza kuwa ATCL
imeboresha huduma zake kwa kiasi kikubwa kwa kuwapatia wateja wake ofa ya
kubeba kilo 20 za mizigo na kilo 7 za mzigo wa mkononi bure pamoja
na kutoa vinywaji na ubadilishaji wa tiketi ni bure ndani ya mwezi.
Aidha, Kaimu Afisa
Mawasiliano wa Kampuni Bi.Lily amekanusha taarifa potofu kuwa zimekwama kuanza
safari zilizopangwa.
Amesema kuwa habari
hizo sio za kweli kwani hivi sasa wameshaanza huduma katika mikoa hiyo mitatu.
Kampuni ya Ndege ya
ATCL kwa sasa ina ndege tatu,zikiwemo mbili aina ya Dash8-Q400 zenye uwezo wa
kubeba abiria 76 kila moja na Dash8-Q300 moja yenye uwezo wa kubeba abiria 50.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...