THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Banda la Tanzania lang’ara maonyesho ya nchini Saud Arabia


Na Mwandishi Wetu, Saud Arabia
MAONYESHO ya biashara na Utalii yaliyoandaliwa nchini Saud Arabia katika Mji wake Mkuu wa Riyadh, yamefanyika wiki iliyopita huku Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikionekana kung’ara baada ya wageni wengi kupendezwa na bidhaa zilizokuwa zinaonyeshwa katika banda la Tanzania.
Katika maonyesho hayo ambayo bidhaa mbalimbali zilionyeshwa ukiwamo eneo maalum la mlima Kilimanjaro, nguo za Kitanzania na viatu pamoja na bidhaa nyingine muhimu zilizoonekana kuwapendeza wengi waliohudhuria maonyesho hayo.
Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Mheshimiwa Hemed Mgaza, alisema kwamba wananchi wengi waliohudhuria maonyesho hayo walionekana kuvutiwa zaidi na nchi ya Tanzania kutokana na vivutio vyake.
Alisema hali hiyo imekuja kutokana na aina ya bidhaa zilizoonyeshwa pamoja na ubunifu wa kutangaza bidhaa zao na nchi kwa ujumla, wakiamini kuwa utachochea wageni wengi wa kutoka nchini hapa kwenda kutembelea nchini Tanzania kwa mambo mbalimbali.
“Binafsi nimefarijika mno kutokana na wenyeji kuandaa maonyesho haya na kutuaalika Watanzania ambao watumishi wa ofisi yangu pamoja na mimi mwenyewe wote tulihakikisha kwamba tunayatumia vizuri kutangaza nchi yetu Tanzania.
“Tumewahakikishia kwamba mbali na nchi yetu kujawa na vivutio vingi kutoka Tanzania Bara na Visiwani, lakini bado tumejawa na amani kiasi kwamba unapokuwa kwenye ardhi ya Tanzania huna sababu ya kuwa na wasiwasi wowote kwa sababu wananchi wake wanaishi kwa upendo,” alisema Balozi Mgaza.
Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, maonyesho hayo kwenye ofisi yao waliyapa jina la Visit Tanzania the land Kilimanjaro, Serengeti and Zanzibar, ambapo pia walitangaza bidhaa za chai, kahawa, viatu vya kimasai, vinyago vya wanyama na nguo za utamaduni.