Mafanikio yaliyopatikana katika ziara za kuhamasisha wafanyabiashara katika mikoa ya Mwanza, Mara na Geita kurasimisha biashara zao, kumelazimu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kufanya zoezi kama hilo katika mkoa wa Simiyu leo.
Baada ya Simiyu, mikoa ya Shinyanga na Tabora itafuata.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Bw. Frank Kanyusi alisema taasisi yake imejipanga kutoa elimu stahili na kuhamasisha wafanyabiashara kujitokeza na kurasimisha shughuli zao.
“Wafanyabiashara katika mikoa hii wajitokeze kwa wingi ili kutumia nafasi hii adimu kwa ufanisi,” alisema Bw. Kanyusi.
Aliwataka wajasiriamali, wafanyabiashara na watanzania wote wa mikoa hiyo wafike kupata elimu ya namna kurasimisha biashara zao na kuzifahamu huduma nyingine zinazotolewa na wakala kwa njia ya mtandao.
Alisema tarehe 3 hadi 8 watakuwa mkoa wa Simiyu, tarehe 10 hadi 15 mkoa wa Shinyanga na tarehe 17 hadi 22 watakuwa mkoa wa Tabora.
Alifafanua kwamba kuna faida nyingi za kurasimisha biashara; ikiwa ni pamoja na kutambuliwa na serikali, kupata fursa mbalimbali, kuwa na walipa kodi wengi na kodi zao kutumika katika ujenzi wa taifa na huduma za jamii.
“Tumeboresha huduma zetu na mtu anaweza kusajili jina la biashara mahali alipo bila ya kufika Dar es Salaam,” alisema Bw. Kanyusi na kufafanua kuwa wengi hawafahamu hilo na kwamba watumie fursa kupata elimu hiyo.
Alisema zoezi katika mikoa ya Mwanza, Geita na Mara ilikuwa ya mafanikioa makubwa kwa vile watu wengi walishiriki na kusajili hapo hapo majina ya biashara kupitia mtandao.
Katika mkoa wa Mwanza, makampuni 100 na majina ya biashara 150 vilisajiliwa; mkoa wa Geita majina ya biashara 60 na makampuni 50 na mkoa wa Mara majina ya biashara 45 na makampuni 30.
Alisema wakala umejipanga kwenda katika mikoa yote nchini kutoa elimu ya urasimishaji biashara na maboresho waliyofanywa ambayo yanatoa fursa huduma kutolewa kwa njia ya mtandao.
Alisema semina hizo pia zinalenga kusikiliza changamoto ambazo zinawakabili wajasiriamali, wafanyabiashara na watanzania wote juu ya huduma zinazotolewa na wakala na kuzifanyia kazi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usajili wa Leseni na Biashara (BRELA), Bw. Frank Kanyusi akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusiana na kuanza kwa mafunzo na zoezi la urasimishaji biashara mkoani Simiyu leo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...