Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
MBUNGE wa jimbo la Chalinze, mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete, ametoa magodoro 50, yenye thamani ya sh.mil 2.225
kwa wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Moreto, waliounguliwa na
bweni lao na kusababisha mali zote kuteketea kwa moto.
Wanafunzi
hao wapatao196, katika shule hiyo iliyopo kata ya Lugoba tarafa ya
Msoga, wilaya ya Bagamoyo, wamenusurika kifo baada ya bweni hilo
kuteketea kwa moto siku ya oktoba 5.
Moto
huo umeteketeza mali zote zilizokuwemo ambazo hadi sasa hazijajulikana
thamani yake.Kufuatia kutokea kwa tukio hilo, Ridhiwani alifika shuleni
hapo kutembelea na kutoa pole kwa kutokea janga hilo.
Alisema
wakumshukuru ni mungu kwani pamoja na kutokea kwa hasara ya kuteketea
kwa mali lakini hakuna madhara kwa wanafunzi yaliyotokea.
Ridhiwani aliwapa pole walimu na wanafunzi kijumla na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kwenda kusaidia pale watakapojaaliwa.
Kwa
mujibu wa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Moreto, Justine Lyamuya
alielezea kuwa, tukio hilo limetokea oktoba 5,majira ya asubuhi ambapo
walianza kuona moshi mzito katika bweni mojawapo wanaloishi wasichana wa
shule hiyo.
Alisema
wakati moto huo unazuka wanafunzi hao walikuwa kwenye masomo yao
darasani."Tulifuatilia na kukuta moto umeshashika kwenye bweni hilo na
jitihada za kuuzima zilishindikana"alisema mwalimu Lyamuya.
Lyamuya
alisema mali zote za wanafunzi wanaolala kwenye bweni hilo zimeteketea
kwa moto hivyo kwa sasa wanafanya tathmini kujua gharama zilizopotea.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani Pwani linafanya uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha moto.
Kamanda
wa polisi mkoani Pwani, Boniventure Mushongi, alielezea kuwa mazingira
ya jengo hilo ni yenye kutumia nishati ya solar power hivyo ni lazima
kufanya uchunguzi wa kina kujua kiini cha kuzuka kwa moto huo.
Alisema bweni hilo linakadiriwa kuwa na wanafunzi 196.
Kamanda Mushongi alisema thamani za mali za wanafunzi katika moto huo bado hazijafahamika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...