Na Nteghenjwa Hosseah, ARUSHA

Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro mwishoni mwa wiki hii amekutana na Maafisa Watendaji wa Kata zote za Jiji la Arusha kuzungumzia kuhusu masuala mbalimbali muhimu yanayotakiwa kupewa kipaumbele katika Wialaya hiii. 

Katika Kikao hicho Dc Daqarro ametilia mkazo masuala ya Usalama wa Chakula katika Mitaa yote, Ulinzi na usalama, usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja na utoaji wa taarifa za matukio yasiyo ya kawaida yanayotokea katika kila Kata.

Akizungumza katika kikao hicho alisema “nahitaji kupata takwimu sahihi kutoka katika kila Kata ya mahitaji ya Chakula, kiasi kilichopo na namna ambavyo mmejipanga kukabiliana na upungufu endapo utatokea, kila afisa ugani wa eneo husika ahakikishe anatoa elimu ya kutosha na kufuatilia kuhusu usalama wa chakula katika eneo lake na kuwasilisha taariha hizo katika Ofisi yangu. Sitamuelewa mtendaji ambaye kwa kutokuwajibika kwake kutasababisha njaa ama upungufu wa chakula kwa namna yeyote ile.

Aidha alisisitiza kusimamia miradi ipasavyo ili iwe na ubora na iweze kudumu muda mrefu, kusimamia Usalama wa Kata kwa kutoa taarifa za kila tukio lisilo la kawaida linalotokea kila siku na kudhibiti uingiaji wa wageni kutoka nje ya nchi wanaofika katika Kata. 

“Wageni wote wa Nje ya Nchi lazima taarifa zao zifikishwe kwa Afisa uhamiaji wa Wilaya ili kujiridhisha kwamba wameingia nchini kihalali na kuwa na shughuli maalumu iliyowaleta katika maeneo yenu aliongeza”.

Sambamba na hilo alisema si ruhusa kwa Mtendaji wa Kata kutoa mihutasarti kwa ajili ya kumilisha upatikanji wa silaha kwa sababu hivi sasa zoezi hilo limesitishwa mpaka pale Uhakiki wa silaha utakapokamilka hivyo kwa kuwa muombaji ni lazima aanzie kwenye ngazi ya kata si ruksa kwa vikao husika kutoa mihutasari ya aina hiyo.

Mwenyekiti wa Watendaji wa Kata katika Jiji la Arusha Ndg. Suleimani Kikingo alisema kwa umoja watahakikisha kwamba maagizo yote yaliyotolewa wanayatekeleza kwa ufanisi ili kuleta mabadiliko ya haraka na kutoa hudma bora kwa wakazi wa Jiji hili.
      Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro akizungumza na Maafisa watendaji wa Kata wa Jiji la Arusha (Hawapo Pichani) wakati wa kikao maalumu na watendaji hao kilichofanyika miwshoni mwa juma jijini hapa.

 Mwenyekiti wa Maafisa watendaji wa Kata na Mtendaji wa Kata ya Kati Ndg. Suleimani Kikingo akichangia wakati wa Kikao na Mkuu wa Wilaya ya Arusha
      Maafisa Watendaji wa Kata waliohudhuria Kikao na Mkuu wa Wilaya ya Arusha

    Afisa Mtendaji wa Kata ya Levolosi Easter Maganza akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali wakati wa kikao


     Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro(kushoto) akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposya wakati wa kikao na watendaji wa Kata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...