Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla jana jioni (Oktoba 13.2016), amekaribishwa na dhehebu la Bohora na kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Bohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin katika msikiti wa dhehebu hilo Upanga Jijini Dar es Salaam.

Mbali na kutoa dua kwa Dk. Kigwangalla, Sheikh Dkt. Syedna ameahidi kuleta wawekezaji wa Kibohora kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi wa Mahospitali ikiwemo Hospitali za Rufaa za kisasa pamoja na Viwanda vya Dawa hali ambayo itapunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kufuata matibabu.

Pia viwanda vya dawa vitashusha gharama za dawa nchini na kupunguza ucheleweshaji unaosababishwa na kuagiza dawa nje ya nchi.

Aidha, katika tukio hilo, usiku huu, Dk.Kigwangalla ameweza kushuhudia ndoa za Vijana zaidi ya 50 zikifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna.

Mbali na Dk.Kigwangalla kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Bohora Duniani, Dkt. Syedna, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba aliungana katika kuombewa na Shehe huyo.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akibusu mkono wa Sheikh Mkuu wa Bohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin isharara ya kupokea dua katika tukio hilo
Waziri wa mambo ya ndani nchini ,Mwigulu Nchemba akiombewa baraka na kiongozi Dawood Bohora Duniani Dkt Syedna Mufaddal Saifuddin katika msikiti wa mabohora Upanga.
Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa tukio hilo.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...