THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

GAPCO KUDHAMINI MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON KILOMITA 10 KWA WALEMAVU

Kampuni GAPCO Tanzania, imetangaza kuendelea kudhamini mbio za Kilimanjaro Marathon 2017 za kilomita 10 kwa walemavu. Akizungumza wakati wa kutangaza udhamini huo jana katika uzinduzi wa mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi alisema Kampuni yake inaona fahari kudhamini mbio hizo za kilomita 10 kwa walemavu.

“Tumeshuhudia mbio hizi za Kilimanjaro Marathon zikikua tangu tumeanza kudhamini mwaka wa 2011 na pia kufurahia faida wanayopata wakimbiaji na jamii inayozunguka maeneo ambayo mbio hizi hufanyika kila mwaka. Tunayo furaha kufanya kazi na Wild Frontiers ambao ndio waandaaji wa mbio hizi, Tanzania Paralympic Committee na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo,” alisema Kakwezi.

Alisema kama njia ya kutoa mchango katika sekta ya michezo na kuendelea kusaidia jamii ambayo GAPCO inafanya biashara, imekuwa mstari wa mbele katika kudhamini mbio za walemavu na mwakani itagharamia usafiri, chakula na malazi kwa washiriki kutoka Dar es Salaam na usafiri kwa washiriki kutoka Arusha. Washindi watapata zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ujumla.

“Kakwezi alisema mbio za Kilimanjaro Marathon zimekuwa maarufu na zinawavutia wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi na hivyo zimesaidia sana kutangaza vivutio vya utalii kama vile mlima Kilimanjaro na kuwaongezea kipato wafanyabiashara wa mji wa Moshi”.

Tunawathamini wateja wetu ambao mchango wao kwa miaka sita umetuwezesha kuendelea kudhamini mbio hizi za kilomita 10 hususani kwa watu wenye ulemavu.

Alisema GAPCO ina matarajio kuwa mbio hizo zitakuwa za kufana na kuwaomba wateja wao kuendelea kutumia bidhaa na huduma za GAPCO ili kampuni iendelee kudhamini shughuli kama hizi.
 Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (wa pili kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon, iliyofanyika jijini Dar es salaam jana.