THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Happy Birthday Mr.President!

Leo 29 Oktoba ndio siku ya Kuzaliwa Rais wetu Dkt.John Pombe Joseph Magufuli. Inawezekana mheshimiwa Rais wetu labda siku hii anaichukulia ya kawaida tu au ya kifamilia tu, kwa kuwanmuheshimiwa si mtu wa kupenda penda ufahari na masherehe. Sikushangaa kumuona leo kavamia Wizara ya Maliasili na Utalii kushuhudia meno ya tembo 50 yaliyokamatwa na kikosi kazi cha kuzuia ujandili. Pia akamtumbua Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI) Athumani Diwani badala ya kukata keki. Lakini pamoja na hayo sisi Watanzania ni lazima tumtakie na kumuombea kila la heri, afya njema Rais wetu  mpendwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika siku ya kuzaliwa - Happy Birthday Mr. President!! YOU ROCK!!
- From Ngoma Africa Band in Germany


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

 1. HK Anasema:

  SIKU YAKO LOZALIWA: (Mh. Rais Wetu John Joseph Pombe MAGUFULI)

  TAREHE LEO MEFIKA, NAO MWEZI KADHALIKA,
  MUHALI SAHAULIKA, IFIKAPO KILA MWAKA,
  NDO SIKU ULOZALIKA, NA KUSHIKA MADARAKA,
  RABI MOLA KUKULINDA, MPENDWA RAISI WETU (JPM).

  MOLA VYEMA AKULINDE, ABADANI TETEREKA,
  MAADUWI UWASHINDE, WABAKI KUADHIRIKA,
  HIYO HIYO SOTE TWENDE, KASI YAKO UNOTAKA.
  RABI MOLA KUKULINDA, MPENDWA RAISI WETU (JPM).

  MWAKA SASA UMETIMU, TANGU WADHIFA KUSHIKA,
  JIKWEZA KWAKO KHARAMU, KHOFU YA MUNGU MEWEKA,
  WATIMIZA MAJUKUMU, HUJALI WANOROPOKA,
  RABI MOLA KUKULINDA, MPENDWA RAISI WETU (JPM).

  KWA WANYONGE MTETEZI, NIA NJEMA UMEWEKA,
  KUPINGA RUSHWA NA WIZI, KOMESHA NA KUTOWEKA,
  MEMA YAKO MAGEUZI, MANUFAA YAONEKA,
  RABI MOLA KUKULINDA, MPENDWA RAISI WETU (JPM).

  TULIA BUKHERI KWAKO, SIKU HII HUKUTAKA,
  UNAJALI NCHI YAKO, KUJUWA YANOTENDEKA,
  ZIARA YA MSHITUKO, MALI ASILI HAZUKA,
  RABI MOLA KUKULINDA, MPENDWA RAISI WETU (JPM).

  WA PEKE WAKO MFANO, KILA KONA WASIFIKA,
  WA PEKE WAKO UONO, TUZO TOKA KWA RABUKA,
  TUNAKUUNGA MKONO, UZI HUO HUO SHIKA,
  RABI MOLA KUKULINDA, MPENDWA RAISI WETU (JPM).

  ILIYOBAKI MINNE, AKUONGOZE RABUKA,
  KILA PENYE GIZA NENE, NURU KWAKO KUIWEKA,
  MAOVU YOTE UONE, UYACHOME KAMA TAKA,
  RABI MOLA KUKULINDA, MPENDWA RAISI WETU (JPM).

  AKUJAALIYE NGUVU, SIHA NJEMA KADHALIKA,
  NA VIONGOZI SHUPAVU, KILA KONA LOWAWEKA,
  WACHAPE KAZI KWA NGUVU, ARI NA KWA UHAKIKA,
  RABI MOLA KUKULINDA, MPENDWA RAISI WETU (JPM).

  TAMATI NAMALIZIAI, TWAKUOMBEA BARAKA,
  FAKHARI KWA TANZANIA, HADI NJE YA MIPAKA,
  MFANO WAKUPIGIA, KWA MEMA UNASIFIKA,
  RABI MOLA KUKULINDA, MPENDWA RAISI WETU (JPM).

  HAPPY BIRTHDAY MR. PRESIDENT!
  THE HON. J.P.J.MAGUFULI.