Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC) imejipanga kuwekeza katika sekta ya viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ili kuchangia kukuza uchumi wa taifa na ajira.

Akifungua Mkutano Mkuu wa 11 wa kampuni hiyo jijiji Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mhandisi Aloys Mwamanga, imejipanga kuanzaisha viwanda vya usindikaji wa mazao ya kilimo, lakini hakutaja idadi ya viwanda na kiasi kitakachotumika. 

Alipoulizwa nje ya mkutano sababu za kuwekeza katika viwanda hivyo, alisema kampuni inaunga mkono kwa dhati dhamira ya serikali ya kuwekeza katika sekta ya viwanda na hasa viwanda vya kusindika mazao. Kampuni imepata faida ya shilingi 564.18 milioni kabla ya kodi.

Bw. Mwamanga amefafanua kuwa kampuni yao ni Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja ambayo imejitokeza kuwa mfano wa kuigwa nchini, na kuongeza kwamba pamoja na ongezeko la gharama za uendeshaji kwa sababu ya kupanuka kwa shughuli za kampuni bado ina uwezo wa kuwekeza. Mwaka 2014 kampuni ilipata faida ya shilingi 784.23 milioni.

Mwenyekiti huyo amesema kwa uwezo iliyonao, kampuni imepanga kuwekeza pia katika dhamana za serekali na makampuni, amana katika mabenki, uanzishaji wa microfinance, ujenzi wa jingo la ofisi na maghala ya kuhifadhi bidhaa.

Alisema uwekezaji huu utakapo kamilika utawezesha wanahisa kupata fedha nyingi zitakazo tokana na gawio la kila mwaka.Amefafanua kuwa kutokana na kushuka kwa thamani ya hisa kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam, mtaji wa kampuni uliathirika kidogo na kupungua kutoka. bilioni 34.56 Desemba 31 mwaka 2014 kufikia bilioni 31.95 Desemba 31, mwaka 2015. 

Kampuni ilipoanza shughuli za biashara Octoba,Mosi, 2005 mtaji wake ulikuwa sawa na bilioni 1.97, alieza Bw. Mwamanga.Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori alisema kampuni inakusudia kujiorodhesha katika Soko la Hisa Dar es Salaam kwa ajili ya kupata mtaji na kufanya uwekezaji zaidi kwa manufaa ya wanahisa na nchi.

“Lengo letu ni kuuza jumla ya hisa 112,500,000 kwa bei ya shilingi 400 kwa kila hisa moja,” na aliongeza kusema kuwa kama hisa zote zitauzwa, watapata bilioni 45.Mmoja wa Wanahisa, Dkt. Tom Maeda, kutoka Hanang, Mkoa wa Manyara ameunga mkono dhamira ya kampuni ya kupanua uwekezaji ili kuongeza mtaji utakao fungua fursa zaidi.

Aliwataka wanahisa wenzake na Watanzania kununua hisa zitakapotangazwa sababu hisa ni uwekezaji ni ukombozi wa mtu anayenunua hisa.Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA ina wanahisa wake 2,443 na ina rekodi ya kufanya mkutano mkuu kila mwaka.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment Plc),Mhandisi Aloys Mwamanga (katikati) akifungua Mkutano Mkuu wa Kumi na Moja (11) wa wanahisa wa kapuni hiyo. (Kulia) ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori na kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Bi. Hanim Babiker. (Picha na mpiga picha wetu, Dr es Salaam).

Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC), Bw. Donald Kamori (kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji kwa mkutano mkuu wa kumi na moja (11) wa kampuni hiyo, ambapo wanahisa walikutana kujadili maendeleo ya kampuni yao, (katikati)ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo,Mhandisi Aloys Mwamanga na kushoto ni Makamu Mwenyekiti,Bi. Hanim Babiker.

Wanahisa wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC) wakifuatilia taarifa ya utekelezaji iliyokuwa ikiwasilishwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC), Bw. Donald Kamori hayupo pichani wakati wa mkutano mkuu wa kumi na moja (11) wa kampuni hiyo. (Picha na mpiga picha wetu, Dr es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...