Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amekemea vitendo vya madalali kula njama na mabenki ili kuuza mali za wakopaji wanyonge kinyume cha sheria.

“Baadhi ya madalali hawafati sheria wanakwenda kwenye minada kutimiza wajibu tu lakini mnunuzi wanakuwa wamekwishapewa,”alisema Lukuvi.

Mhe. Lukuvi ameyasema hayo leo katika kikao na madalali kilichofanyika jijini Dar es salaam ili kuwaonya madalali wasio waaminifu.

Akizungumza katika kikao hicho, Lukuvi amesema amepokea zaidi ya kesi 80 za watu walioonewa na madalali hao, na kati ya kesi hizo zaidi ya asilimia 75 ni wanawake.

Aidha, Waziri Lukuvi amesema kuwa suala hili halikubaliki ambapo thamani ya mali inayouzwa huwa ni siri kati ya dalali na benki wakati mwenye mali hajui na amefichwa makusudi. “Bei zinazouzwa huwa ni chini sana hadi kufikia alimia 50 mpaka kushuka hadi 25 ya tamani ya nyumba au kiwanja, hii ni sawa mchezo huu uachwe mara moja,” alisema Lukuvi.

Sheria imeelekeza mkopeshaji kujali maslahi ya mkopaji kabla ya kuuza dhamana. Imeelekeza mali au dhamana inayotakiwa kuuzwa isiuzwe chini ya ailimia 75 ya bei ya soko lililopo wakati huo, alisema Lukuvi.

Amebainisha kuwa baadhi ya maafisa wa benki hupanga njama kwa lengo la kujiuzia mali hizo kwa bei ya chini. Lukuvi ameonyesha kusikitishwa kwake na vitendo hivi viovu na kusema katika zoezi hili wajane na watoto wa maskini hunyanyasika na kuumizwa sana.

“Nyumba yenye thamani ya  shilingi 432,000,000 huuzwa kwa 140,000,000 na bado anatakiwa kulipia gharama nyingine. Kadhalika shamba lenye thamani ya shilingi bilioni 1 linauzwa kwa milioni 200 wakati mkopo halisi ulikuwa milioni 400,”alifafanua Lukuvi.

Lukuvi amesema kuwa nataka sasa kukomesha wizi huo wa mchana eti kwa kisingizio cha sheria. “Kuanzia sasa Wizara yangu haitabadilisha hati (Transferring)  ya nyumba au ardhi hadi ipate taarifa kamili ya mwenendo wa uuzaji kama umefuata sheria”, alisisitiza Lukuvi.

Vimekuwepo vitendo vya baadhi ya madalali hapa nchini vya kuwanyanyasa wakopaji walioshindwa kurejesha mikopo yao kwa wakati. Hivyo Wizara imeamua kuingilia kati ili kukomesha vitendo hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...