Benny Mwaipaja, MoFP-Washington DC, Marekani

MAWAZIRI wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi mbalimbali za kiafrika, wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, wamekutana Jijini Washington DC, Marekan,i na kuzitaka Taasisi hizo kuweka mipango inayoakisi na kutatua changamoto zinazolikabili bara hilo ikiwemo, uhalifu, umasikini, mizozo ya kivita na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi

Aidha, Viongozi hao wamezitaka taasisi hizo kuweka uwiano wa uwakilishi wa uongozi wa juu ili kuhakikisha kuwa maslahi mapana ya nchi hizo yanalindwa na maendeleo endelevu yanafikiwa kwa haraka.

Akizungumza kwenye moja ya mikutano hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ambaye kiutaratibu ni mmoja wa Magavana wa Benki ya Dunia na IMF, amesema kuwa mashirika hayo ya fedha ya kimataifa yanamchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania.

Hata hivyo amesema kuwa mdororo wa uchumi duniani, ambao unaonesha kuwa viwango vya ukuaji wa uchumi vilivyokadiriwa kufikiwa kwa asilimia 3, havitafikiwa ambapo takwimu zinaonesha kuwa ukuaji wake hivi sasa ni asilimia 1.5 tu, unaashiria namna nchi wanachama zinatakiwa kujipanga kuhakikisha kuwa uchumi unapanda.

Dkt. Mpango amesema kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kwa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka lakini changamoto kubwa iliyopo ni kuhakikisha kuwa uchumi huo unaonekana katika maisha ya kawaida ya wananchi wake. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Katibu Mkuu Bw. Dotto James (kulia) wakiandika pointi muhimu wakati Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim, alipowahutubia Mawaziri wa Fedha na Makatibu wakuu (Magavana) kutoka nchi za Kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, Jijini Washington DC-Marekani. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Fedha wa Swaziland kushoto kwake walipokuwa kwenye mkutano na  Mkurugenzi Mtendaji Bi. Christine Lagarde Jijini washington DC- Marekani. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, Kanda ya Afrika, Bi. Chileshe Mpundu Kapwepwe Hayupo pichani), Jijini Washington DC-Marekani. Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu akifuatiwa na Naibu Gavana wa Benki hiyo Dkt. Natu Mwamba.
 Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Hiroshi (Hiro) Kato, akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kitabu Chenye maelezo mbalimbali ya miradi inayotekelezwa nchini Tanzania kwa ufadhili wa shirika hilo, ambapo Japani imeahidi kuendelea kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kuendeleza miundombinu ya barabara na sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
(Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango) 

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...