Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost,  Rachel Mwalukasa (kushoto), akizungumza wakati wa  mahafali ya pili ya kidato cha nne ya shule hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias mkoani  Pwani hivi karibuni. Wengine kutoka  kulia ni Mkuu wa Shule, Alex Nicholaus, Mhadhiri kutoka  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Dk Ellen Kilinga na Mhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya UDSM (COICT), Dk Suzan Lujara aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo. 
 Mhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya UDSM (COICT), Dk Suzan Lujara (wa pili kulia) akimpongeza Mohamed Ibrahim, mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri kimasomo na kujizolea kutwaa tuzo mbalimbali wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha nne ya shule hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias, Pwan​i hivi karibuni. Wengine kutoka Kulia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM, Dk Ellen Kilinga, Mkurugenzi Mtendaji was Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa na Mkuu wa shule hiyo, Alex Nicholaus.  
Wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost wakipozi katiaa picha ya kumbukumbu pamoja nja baadhi ya walimu, viongozi wa shule na mgeni rasmi wakati wa  mahafali yao shuleni hapo, Kihaba, Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...