THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAJAJI WAPONGEZWA KWA KUMALIZA VIZURI KESI ZA UCHAGUZI


Na Lydia Churi-Mahakama

Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Majaji wengine wamepongezwa kwa kumaliza vizuri kesi za uchaguzi zilizofunguliwa katika Mahakama Kuu kanda mbalimbali nchini na pia kutenga muda wa kujadili changamoto zilizotokana na kesi hizo.

Akizungumza na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania leo jijini Arusha, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amewapongeza Majaji hao kwa kujitoa katika kusikiliza kesi hizo na kuzitolea hukumu kesi nyingi kwa kipindi kifupi licha ya kesi chache kubakia mahakamani.

Jumla ya kesi 53 za Ubunge zilizotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 zilifunguliwa katika Mahakama Kuu kanda za Dar es salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya, Moshi, Mtwara na Mwanza. Kanda nyingine ni Shinyanga, Songea, Sumbawanga, na Tanga. Kati ya kesi hizo, kesi 31 zilimalizika katika hatua za awali na kesi 22 ziliendelea, mpaka sasa kesi 19 zimemalizika. kesi tatu bado ziko mahakamani.

Hata hivyo kesi zote 196 zilizotokana na uchaguzi wa madiwani zilimalizika mapema katika Mahakama mbalimbali za Hakimu Mkazi nchini. Katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi Mkuu nchini, zaidi ya asilimia 94 ya kesi za uchaguzi zilizofunguliwa kwenye Mahakama Kuu zimemalizika wakati asilimia 100 ya kesi zote za udiwani zimemalizika.

Aidha, Jaji Mkuu amewataka Majaji hao kuweka mikakati ya kuhakikisha kasi ya kupunguza kesi mahakamani hasa zile za muda mrefu inaongezeka ili kupunguza malalamiko yanayotokana na kuchelewa kutoa hukumu na kutopatikana kwa nakala za hukumu kwa wakati.

Mheshimiwa Chande amewataka Majaji kusimamia suala la maadili ndani ya Taasisi hiyo ili kurejesha imani ya wananchi kwa Mahakama yao.

Kuhusu suala la Maadili kwa Mahakimu, Jaji Mkuu amesema wameomba ushauri Tume ya Utumishi wa Mahakama kuwa endapo hakimu atashtakiwa kwa kosa la rushwa ataondolewa kazini kwa maslahi ya Umma hata kama atashinda kesi hiyo.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akizungumza na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (hawapo pichani) leo jijini Arusha. Katika Mkutano huo, Jaji huyo aliwapongeza Majaji kwa kuziendesha vizuri kesi zilizohusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015PICHA NA LYDIA CHURI-MAHAKAMA .