THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAKALA YA SHERIA: NANI ANASTAHILI KIPAUMBELE KUSIMAMIA MIRATHI KATI YA WARITHI WA MAREHEMU

Na  Bashir  Yakub.

Ni vema  kujua nani  anapaswa  kupewa  kipaumbele  cha  kusimamia  mirathi  pale   mwenye  mali  anapokuwa  ameaga  dunia. Mara  kadhaa  mjadala  huibuka   baina  ya  wanafamilia  hasa  pale  inapotokea  kuwa  marehemu  alikuwa  na  mke  zaidi  ya  mmoja  na  kila  upande  kuna  watoto. 

Lakini  pia  hata  pale  marehemu  anapokuwa  na  mke  mmoja  mjadala  huu  napo  waweza  kuibuka  kati  ya  wanaotegemewa  kurithi  juu  ya  nani  awe  msimamia  mirathi. Hii  si  pale  tu  anapokufa  baba  lakini  pia  hata  panapo mswiba wa mama  mjadala huu huibuka.

1.WOSIA  KUTAJA  MSIMAMIA  MIRATHI.
Ikiwa  marehemu  ameacha  wosia  na  katika  wosia  huo  imeelezwa  wazi  nani  atakuwa  msimamizi wa  mirathi  basi  huyo  aliyetajwa  ndiye  atakuwa  msimamizi  wa  mirathi . Wosia  unaweza kumtaja  mtu  mmoja kusimamia  mirathi  au  zaidi  ya  mtu  mmoja. Kwa  vyovyote  utakavyotaja   hao  waliotajwa  ndio  watasimamia  mirathi.

2.  WOSIA  KUTOTAJA  MSIMAMIA  MIRATHI.
Si  wakati  wote  wosia hutaja  msimamia  mirathi.  Hii  yaweza  kutokea  kwa  kutokujua  kwa  aliyeandika wosia   au  kujua  lakini  kuacha  makusudi  kwasababu  nzuri  anazozijua  mwenyewe.  Kwa  namna  yoyote  itakavyokuwa  wosia  usipotaja nani   asimamie  mirathi  basi   ni  wajibu  wa  wanafamilia  kuhakikisha  anapatikana    msimamizi ili  agawe  mali kutokana  na  wosia  unavyoeleza.

Muhimu  ni  kuwa  ni  lazima  apatikane  msimamizi   wa  mirathi.  Aweza  kuwa  mmoja  au  zaidi. Swali  kwetu  ni  ikiwa  kumetokea mgogoro  kuhusu  nani  asimamie  mirathi  je  nani  afaa zaidi  kuliko wenzake  kupewa  kipaumbele  kwa  mujibu  wa  sheria.

3.NANI APEWE KIPAUMBELE  CHA KUSIMAMIA  MIRATHI  KATI  YA  WARITHI   WA  MAREHEMU.
Sura  ya  352  ya  sheria  ya  usimamizi  mirathi  ndiyo  huongoza  jambo  hili.  Ikumbukwe  tumesema  hapo  juu  kuwa  suala  la  nani apewe  kipaumbele  cha  kusimamia  mirathi  linaibuka  pale  tu  ambapo  marehemu  hakuacha  wosia  kabisa  au  ameacha  wosia  lakini  ndani  mwake  hakumtaja  msimamizi  wa  mirathi.